Mbatia: Sijatumwa na Magufuli kuiangusha CHADEMA Mbeya

mbona siasa zilikatazwa nani kampa kibali cha kuzunguka huko
 
Mbatia kafika mwisho kama mrema.. watu wa vunjo wana matatizo sana.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, John Magufuli ya Machi 3, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam hayakulenga kukiangusha Chadema katika majimbo ya Rungwe, Busokelo na Kyela katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

"Nimekuja Mbeya kwenye ziara ya kukiimarisha chama cha NCCR si kwamba nimetumwa na Rais John Magufuli kuja kukiua Chadema. Hiyo ni hofu yao, majungu na ufike wakati kujenga hoja za fikra,” amesema Mbatia leo Jumamosi Machi 7, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mbeya.

Amebainisha kuwa ziara yake mkoani humo ni kwa ajili ya kukiimarisha chama na kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi katika majimbo hayo.

Machi 3, 2020 katika kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni kuibua matumaini mapya ya maridhiano, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa vyama vya upinzani Ikulu, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kuhimiza haja ya kudumisha amani, usalama na upendo.

Viongozi waliokutana na Rais kwa nyakati tofauti ni mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad; Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba na Mbatia.

Hata hivyo, haikueleweka mara moja kama kukutana huko kutakuwa na mwendelezo wa vikao vingine vya viongozi wengine wa upinzani.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa alipoulizwa kwa simu alisema suala hilo ni siri ya ratiba za rais.

Baada ya asubuhi viongozi hao kukutana na Rais, mchana Mbatia alikutana na waandishi wa habari na kumpokea katibu mwenezi wa zamani wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Edward Simbeye na kisha kutangaza kuanza ziara ya kukiimarisha chama hicho.

Katika mkutano wa leo, Mbatia amesema, “nimefanya ziara katika jimbo la Rungwe, Busokelo na Kyela kimsingi nimejionea hali halisi barabara mbovu, uchafu na kwetu sisi kama NCCR tunataka kusimamisha wagombea katika nafasi zote za udiwani, ubunge na urais ili kujenga utu, ujamaa na umoja wa Watanzania.”

Mbatia amesema vyama vya siasa nchini vinajidanganya kama ni bora kuliko vyama vingine na kwamba hakuna chama wala serikali yenye nchi, “bali kila chama kina haki ya kushika dola na kuongoza wananchi na ndio maana mwalimu Nyerere (Julius) aliingiza mfumo wa vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana na hoja na si matusi, kejeli na propaganda zisizo na maslahi mapana kwa Watanzania.”

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbatia atayamalizia maisha yake kwa aibu kubwa. Atakosa utu na heshima mbele ya jamii. Atadharaulika na wananchi, vyama vya upinzani na CCM pia.

Kazi aliyopewa Mbatia ni ngumu. Na aliyempa hiyo kazi, na resources, atakapoona mtu ambaye amepa kazi na yeye kuahidi ataweza, halafu hawezi kuleta matokeo aliyoyaahidi, atamdharau zaidi.
 
Njaa Kali haina mjanja! Kati ya hao watatu ni mmoja ninayeweza kumwamini! Huyo mmoja alitengua nanihii yake kwa lengo LA kuvuruga na akafanikiwa, kisa alitumwa ! Huyo mwingine aliwahi kuwa mjengoni kwa fadhila za kijani! Hapo unategemea nini? Yule malimu anavutwa tu na pia anaonekana kujikatia tamaa!!
 
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, John Magufuli ya Machi 3, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam hayakulenga kukiangusha Chadema katika majimbo ya Rungwe, Busokelo na Kyela katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

"Nimekuja Mbeya kwenye ziara ya kukiimarisha chama cha NCCR si kwamba nimetumwa na Rais John Magufuli kuja kukiua Chadema. Hiyo ni hofu yao, majungu na ufike wakati kujenga hoja za fikra,” amesema Mbatia leo Jumamosi Machi 7, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mbeya.

Amebainisha kuwa ziara yake mkoani humo ni kwa ajili ya kukiimarisha chama na kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi katika majimbo hayo.

Machi 3, 2020 katika kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni kuibua matumaini mapya ya maridhiano, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa vyama vya upinzani Ikulu, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kuhimiza haja ya kudumisha amani, usalama na upendo.

Viongozi waliokutana na Rais kwa nyakati tofauti ni mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad; Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba na Mbatia.

Hata hivyo, haikueleweka mara moja kama kukutana huko kutakuwa na mwendelezo wa vikao vingine vya viongozi wengine wa upinzani.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa alipoulizwa kwa simu alisema suala hilo ni siri ya ratiba za rais.

Baada ya asubuhi viongozi hao kukutana na Rais, mchana Mbatia alikutana na waandishi wa habari na kumpokea katibu mwenezi wa zamani wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Edward Simbeye na kisha kutangaza kuanza ziara ya kukiimarisha chama hicho.

Katika mkutano wa leo, Mbatia amesema, “nimefanya ziara katika jimbo la Rungwe, Busokelo na Kyela kimsingi nimejionea hali halisi barabara mbovu, uchafu na kwetu sisi kama NCCR tunataka kusimamisha wagombea katika nafasi zote za udiwani, ubunge na urais ili kujenga utu, ujamaa na umoja wa Watanzania.”

Mbatia amesema vyama vya siasa nchini vinajidanganya kama ni bora kuliko vyama vingine na kwamba hakuna chama wala serikali yenye nchi, “bali kila chama kina haki ya kushika dola na kuongoza wananchi na ndio maana mwalimu Nyerere (Julius) aliingiza mfumo wa vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana na hoja na si matusi, kejeli na propaganda zisizo na maslahi mapana kwa Watanzania.”

Chanzo: Mwananchi
Tunakushukuru sana bwana mbatia kwa kupandishwa cheo kwenye kazi yako ya usaliti ENDELEA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKO SISI TUACHIE MAMA TANZANIA😂😂😂
 
Comrade Mbatia,
Nadhani huenda hujasoma alama za nyakati - kiukweli chama chako kimekufia (yaaaaani huwezi kukaa sehemu yoyote kisha ukasikia hata mtu akikitaja)

Nafasi ya CUF na NCCR imechukuliwa na ACT Wazalendo (Mbatia kuna mahali ulikwama kimkakati)
 
Hakuna mwenye hati miliki na mkoa wowote hapa tanzania, kila mtu anayo haki ya kwenda popote katika jamhuri hii.
 
Fedha zinazotumiwa na gvt kuididimiza Cdm ni Mara 5 ya fedha zinazotumiwa na cdm yenyewe kujiimarisha hakika chama hiki kipo juu ya imara
 
Back
Top Bottom