Mbegu aliyotupa baba haileti Mavuno

Mbegu aliyotupa baba haileti Mavuno

Taric Hiyari

Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
5
Reaction score
3
Hakuna Mkulima yoyote Duniani anayepanda mbegu fulani na kutegemea aje kuvuna Mabua, hivyo ndivyo ilivyo hata katika Maisha yetu ya leo,

Mfano mzuri ni wale wote wanaoshiriki katika Uandikaji wa hizi stori za Mabadiliko, wanapanda Mawazo na Fikra mbalimbali zinazowazunguka katika Maisha yao kwa malengo yanayotofautina, wengine wakilenga zaidi katika kuijenga jamii kutokana na Mawazo yao ili kuvuna kizazi kilicho bora,

Wengine pia wakitaka kuvuna zile zawadi ama tuzo zilizoandaliwa kutokana na kile walichokiandika ama kukipanda, Hivyo ndivyo watu wanavyotofautina katika Upandaji wa vile wanavyovipanda na katika kuvuna vile wanavyotaka kuvivuna katika Maisha ya kila siku, Lakini mbegu Sharti ikomae na kufikia hatua ya kupandwa ili ije kuzalisha mbegu nyingine iliyobora, huchukua kikomo fulani cha Muda mpaka iweze kufika hatua ya kupandwa na kuweza kukua na kua mti kamili wenye kuzalisha Miti yenye mbegu nyengine.

Na hapa ndio Misingi wa Mambo yote Duniani yanapoanza Kwa mtu mmoja mmoja, kundi fulani la watu na hata jamii kwa Ujumla, Tunashindwa kupanda zile mbegu tunazozihitaji katika kipindi sahihi tunachokihitaji na kupelekea kuvuna Mabua, kwa kua mbegu zetu tunazozipanda hazileti Mavuno yale tunayoyahitaji na kuleta Ustawi mdogo katika Maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na hata jamii kwa Ujumla na ndio Maana hata Matunda yake inakua ni ngumu kuwafikia walaji,

Hukaa kwa mda mchache na Kuoza na hata thamani yake ni ndogo Mno na kuna Utofauti Mkubwa wa mbegu zilizozalishwa katika zama zile na zama za hivi leo kwa maana zilikua ni za Uhakika na kuaminika na kudumu Muda mrefu hata zikichanganywa na kundi jingine la Mbegu tofauti na hizo, na Mavuno yake yalikua ni ya uhakika na kutegemewa na watu wote katika jamii na hata nje ya mipaka, na ndio maana zilituwezesha kutufikisha leo hapa tulipofika ,

Nikikaa peke angu huwa najiuliza Je hizi Mbegu za kisasa zitaweza kutufikisha kweli pale tunapopataka na kupahitaji ?

Basi kichwa hubaki tu kikiniuma kutwa kucha maana hata Umwagiliaji wake ni hafifu na haukidhi vigezo vya pale tunapotakiwa kutoka na kwenda ama kufika pale tunapopahitaji kuwepo.
 
Back
Top Bottom