Mbegu Tunayoipanda Ndiyo Tutakayoivuna - Siku Zote Tujitahidi Kupanda Mbegu Bora na Njema

Mbegu Tunayoipanda Ndiyo Tutakayoivuna - Siku Zote Tujitahidi Kupanda Mbegu Bora na Njema

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,499
Reaction score
5,956
Hello JF Members,

Ujumbe wangu upo ndani ya hii story fupi.

Kulikuwa na mama mjane, maskini sana, aliyeishi na watoto wawili wadogo kijijini. Mama huyo alikuwa mchuuzi wa mbogamboga. Kila siku, alihangaika kupata angalau shilingi 500 ili apate unga wa jioni.

Siku moja, mama aliuza mboga zake akapata shilingi 500 kama kawaida. Akiwa njiani kurudi nyumbani, alipita mbele ya duka la vitabu na akakiona kitabu cha hesabu kilichohitajika shuleni kwa mwanae Mkubwa. Kilikuwa kinauzwa shilingi 500.

Alisimama, kisha akaitazama hela aliyonayo mkononi, mkononi. Akageuka pembeni kutazama duka la chakula, Kisha la vitabu. Akafumba macho kwa Sala fupi, kisha akaingia dukani na kununua kitabu.

Usiku ulipofika, watoto wake wakamwambia: “Mama, leo tunakula nini?”

Mama akawashika mikono na kumkabidhi kitabu yule Mkubwa kitabu.
“Leo hatutakula chakula cha tumboni, lakini tutakula cha kichwani. Elimu itawashibisha miaka mingi ijayo wanangu.”

Watoto walilia kwa njaa, lakini hawakusahau jambo hilo. Waliapa mioyoni mwao kuwa watasoma kwa bidii ili mama yao asiwahi kulala njaa tena.

Miaka ilipita na watoto wale, mmoja akawa daktari bingwa. Siku ya uzinduzi wa hospitali yake, alisimama na kusema: “Mama alinipa kitabu mikononi badala ya chakula mdomoni. Ndio maana leo nimenunua chakula na vitabu kwa wengine, maana angenipa chakula Cha tumboni ningekosa cha akilini na nisingekuwa hapa.”

Ukipanda Mbegu katika Mema utavuna mavuno mema.

Kumbuka, njaa mara nyingi ni mwalimu bora kuliko shibe; kwa sababu katika nyakati ambazo hukupata chakula cha mwili, akili yako ililazimika kuchambua mambo kwa kina na kutafakari kwa upana zaidi ili kupata ufumbuzi.

TUSICHOKE KUJITOLEA NA HATA TUKIKOSA MKATE WA SIKU TUSIMKUFURU MUNGU WETU, MAANA MUNGU ANAWEZA KUPANDA WAZO LA UTAJIRI WA MILELE LINALOWEZA KUKUTOA KWENYE UMASKINI NA NYAKATI NGUMU DAIMA.

TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO NA UBARIKIWE SANA.
 
Back
Top Bottom