shelumwa
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 516
- 189
[HASHTAG]#NGUVUzaKIUME[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TUELIMISHANE[/HASHTAG]
UNAIFAHAMU MBEGU YA KIUME ILIYO BORA NA YENYE UWEZO WA KUTUNGISHA MIMBA? twende pamoja
Kama kila ukifanya tendo la ndoa, mwanamke anatoka shahawa/mbegu dakika chache mara baada ya kumaliza tendo la ndoa hata kama hajasimama>> Iyo ni dalili mojawapo mbegu za kiume sio bora - soma hadi mwisho mada hii nzuri ili kujua kiundani na suluhisho
UBORA WA MBEGU ZA KIUME (SPERM ANALYSIS). Kawaida kazi ya kuichunguzi wa UBORA WA MBEGU ZA KIUME hufanyika katika hospitali ambapo mbegu zako za kiume huchukuliwa na kisha kuchunguzwa na daktari mzoefu. Sote tunajua wazi ya kwamba unaweza fanya tendo la ndoa kila siku za hatari na bado usitungishe mimba. Tatizo linaweza kuwa kwa mama au baba au wote wawili. Tumesha yaelezea sana matatizo haya katika mada nyingi ziilizopita hapahapa. Kwa upande wa baba kuna wakati unaweza JITAMBUA KAMA huna mbegu bora kutokana na muonekano wa manii/shahawa zako pamoja na kiasi cha shahawa kinachotoka katika kila tendo moja.
HAPA ILI UJIFUNZE MACHACHE
1- UWINGI WA MBEGU ZA KIUME: Mbegu za kiume katika kila tendo kamilifu moja linalofanywa zinatakiwa zisispungue milioni 40. Kiasi hiki sio rahisi kukijua kwa macho yako. Lakini ikiwa utatoa shahawa kidogo, kuna uwezekano wa kuwa na mbegu za kiume chache. Ingawa sio mara zote utoapo shahawa chache basi humaanisha una mbegu chache. Mshindo dhaifu au kufika kileleni kirahisi rahisi ni mojawapo ya dalili ya kwamba mbegu unazotoa sio nyingi, inaweza kuwa na maji mengi badala ya kuwa na mbegu nyingi.
2- UZITO WA MBEGU ZA KIUME NA UWEZO WA KUCHELEWA KUYEYUKA – Shahawa/majimaji ya mbegu huwa na mbegu za kiume, na shahawa ni majimaji yanayobeba mbegu za kiume, kazi ya shahawa ni kusafirisha kwa usalama mbegu za kiume mpaka kulifikia yai. Sasa ikiwa shahawa zitakuwa nyepesi (zina yeyuka haraka) basi maana yake kwa haraka sana baada ya kutoka uumeni shahawa na mbegu za kiume zinatengana, na hivyo kuathiri uwezo wa mbegu kusafiri haraka na kulifikia yai. Mfano mdogo ni kwamba kama ukishafanya kitendo cha ndoa na kisha muda huohuo mbegu za kiume kuanza kuchuruzika kutoka nje ya uke hata kama mwanamke amelala basi hiyo ni dalili mojawapo ya mbegu kuwa nyepesi na hivyo kuweza kuathiri uwezo wa kutungisha mimba. Kunaweza kuwa na matatizo mengine ya uko kutoweza kushikilia vizuri mbegu za kiume pia, hiyo nayo inaweza kuwa sababu.
3- UWEZO WA KUOGELEA KWA KWENDA MBELE – Mbegu za kiume zenye afya bora zinakichwa kikubwa kilichochongoka na mkia mrefu unao anza mkubwa kichwana na kuishia mdogo kabisa mkiani, sifa hizi zinazipa mbegu uwezo wa wa kuogelea kwenda mbele katika mstari mnyoofu, ikiwa mbegu ya kiume itasafiri katika mstari wa zigzig au maumboumbo basi inapoteza uwezo wa kufika haraka kuliwahi yai. Hii ni kwa sababu zinachoka. Mbegu zinazoenda katika mstari mnyoofu zinawahi kufika kwa kuwa safari inakuwa fupi. Mfano mzuri ukisafiri na nedge toka Mwanza hadi Dar na Mwingine Asafiri na Train na mwingine na Bas utakuta wanafika muda tofauti na pia wanakuwa wamesafiri umbali tofauti kabisa. Ndivyo ilivyo kwa mbegu zinazoogelea kwa mwendo wa nyoka na zile zinazoogelea kwa kwenda mbele moja kwa moja
4- UWEZO WA KUISHI – Mbegu bora inafaa iishi sio chini ya masaa 72 tangia itoke kwa mwanaume na kuingia kwa mwanamke, maisha mafupi ya mbegu yanaifanya mbegu kuwa na wakati mgumu wa kuliwahi yai ili kulitungisha mimba.
5- RANGI – Kawaida shahawa zenye mbegu bora zina rangi nyeupe inayoelekea kwenye gray na kwa wazee inakuwa nyeupe inaelekea njano – Sasa huwezi ona rangi hii mara kwa mara kwa sababu mbalimbali za kiafya, chakula na hali ya hewa. Lakini kwa watu wazima miaka 40 kwenda juu ni kawaida sana mara nyingi kuonekana nyeupe/njano.
NINI CHA KUFANYA IKIWA UNAONA DALILI HIZI?
Ukiona dalili hizi au kama umepima na kukutwa na dalili hizi, na ikiwa katika ndoa yako upatikanaji wa mimba imekuwa ngumu, na ikiwa pia mama mara kwa mara hujikuta na mbegu za kiume zinamtoka na kuchuruzika muda mchache mara baada ya tendo la ndoa basi tambua ya kwamba ubora wa mbegu zako ni mdogo na kwa iyo unahitaji utatuzi wake.
[HASHTAG]#KWANZA[/HASHTAG] BORESHA MBEGU ZAKO ZA KIUME kwa kula chakula chenye zinki kwa wingi mfano mbegu zote za matunda na maboga zinazolika, zina zinki na madini ya chuma kwa wingi. Hakikisha hukosi hizo mara kwa mara, ikiwa umeathirika zaidi au tuseme umetumia muda mrefu zaidi ya mwezi na huoni mabadiliko basi huna budi kupata dawa za hospitalini au kupata virutubisho na madini kutoka katika wasambazaji walio thibitishwa.
[HASHTAG]#PILI[/HASHTAG] ACHANA NA TABIA MBAYA ZINAZOWEZA KUWA SABABU YA MBEGU KUWA DHAIFU mfano ulevi wa kupingukia, sigara, madawa ya kulevya, punyeto, ngono kinyume na maumbile,kutokula chakula vizuri, madawa ya kulevya na kukosa kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
TATU JITIBU MAGONJWA SUGU – Huu umekuwa wimbo wa taifa, nadhani unakumbuka pia ya kwamba sasa waziri ametoa tangazo la watu kufanya mazoezi mara kwa mara. Magonjwa ya kitabia kama kisukari, presha na matatizo ya ini na figo ni kiashiria tosha ya kwamba mifumo ya mwili imechoshwa na kuzeeshwa na vyakula vibaya tunavyokula. Kwa hivyo ni muhimu kujitibu magonjwa hayo haraka