Mbegu za tikiti maji zina faida gani mwilini ?

Mbegu za tikiti maji zina faida gani mwilini ?

Danos

Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
89
Reaction score
104
Ndugu wana jukwaa, habari za muda huu ?. Ninaomba kufahamishwa faida za mbegu za tikiti maji(water melon) kwa matumizi ya mwanadamu. Mwenye ujuzi kuhusu hili anifahamishe. Naomba kuwasilisha.
 
Kazi kubwa ya mbegu za tikiti maji mwilini ni kuongeza nguvu za kiume. Jaribu kula tikiti na mbegu zake kama wiki au wiki 2 mfululizo na utaniambia

560055_628560130540734_2001384276_n.jpg
 
Fadhili Paulo, na nguvu za kike je? Maana mie naonaga uvivu kuzitema nameza nisije haribu mambo. Kama ujuavyo nguvu za kike (+ve) na za kiume (-ve), ukiziunganisha zinaweza kukanseliana.
 
Last edited by a moderator:
Fadhili Paulo, na nguvu za kike je? Maana mie naonaga uvivu kuzitema nameza nisije haribu mambo. Kama ujuavyo nguvu za kike (+ve) na za kiume (-ve), ukiziunganisha zinaweza kukanseliana.

Hata mimi zamani nilikuwa nazichukia na kila ninapokula tikiti nilikuwa nazitengenisha kabisa hizo mbegu, lakini nilipokuja kujuwa thamani yake nikaanza kuzitafuna tena kwa fujo, amini usiamini dawa tunazo majumbani mwetu ila hatuzijuwi tu.

Wewe zitumie na pia mpe na mr naye azitumie wote mtakuwa sawa.



Kutoka mwanachi:

Faida za tikikiti maji kiafya

tikiti.jpg


Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.

Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.

Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.

Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:

Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.

Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.

Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.

Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.


Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.


Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake na mbegu zake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.


Kwa kawaida tunda hili huliwa pejke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.
 
Aisee, faida zake nyingi zaidi ya upatikanaji wake.
Bora kila familia iwe na mmea wa tunda hili kabisa!
 
Ni kweli niliona tofauti kubwa baada ya kuanza kutumia juice ya tikiti maji mara kwa mara bila kugundua. Baada ya kusoma Mahali kua punje zake zinaongeza hayo makitu ndio nikaja kuprove. Sababu huwa nasaga na punje zake. Kero yake ni kwenda haja mdogo mara kwa mara unapotumia juice hii.
 
Ni kweli niliona tofauti kubwa baada ya kuanza kutumia juice ya tikiti maji mara kwa mara bila kugundua. Baada ya kusoma Mahali kua punje zake zinaongeza hayo makitu ndio nikaja kuprove. Sababu huwa nasaga na punje zake. Kero yake ni kwenda haja mdogo mara kwa mara unapotumia juice hii.

Kazi yake ni kutoa sumu mwilini, na sumu hutoka kupitia njia ya mkojo
 
Asanteni sana wadau kwa michango yenu mizuri.
 
Uzi kama hiz mmepandisha sana bei za tikit maji
 
Back
Top Bottom