Mbegu zipi za mahindi za DK zinafanya vizuri?

Joined
Oct 27, 2021
Posts
61
Reaction score
113
Wanajamii habari zenu wote.

Polen wadau kwa Mihangaiko za hapa na pale, Ndugu zangu najua huku kuna wakulima wazuri japo wapo pia paper farmers lakini najua mkulima wakweli akitoa ushauri huwa tunamwelewa kwasababu huwa anatoa uhalisia wa mambo ambapo hata msomaji anarithika kabisa.

Ndugu zangu naombeni mnisaidie kunipa mwanga ni mbegu gani aina za DK (DK varieties) hutoa mavuno mazuri na pia hustahimili hali ya hewa ya joto kali ukiongezea pia na mabadiliko ya hali ya hewa ya miaka hii.

Binafsi nimeshawahi kujaribu kutumia DK8031 na DK8033 mwaka jana ilikuwa nzuri japo mwaka ulikuwa siyo poa. mwaka huu natamani kujaribu aina nyinginezo za DK lakini nategemea wadau mnipe mwongozo mzuri. eneo la shamba ni Kilindi -Kibirashi mkoa wa Tanga

Asanteni 🙂
 
DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni bora za kilimo.
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutosha bado hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave".
 
Gunia 40 kwa heka moja?
 
Hawa ndo wale wakulima ambao wamesomea tu hawajawahi kulima hata mahindi ya kikombe Kimoja
Shida yenu mnalima km babu zenu walivyolima ndio maana kila kitu hamuamini. We mtu unapanda ovyo ovyo, hauzingatii idadi ya mimea kwa ekari, shamba kubwaa mimea michache, hufanyi palizi kwa wakati, mbolea unaweka mara moja, toka babu hadi mjukuu shamba halijawahi rutubishwa kwa mbolea za asili kwanini usivune gunia 8 kwa ekari?

Hizo gunia 40-44 unazipata km shamba litakua na rutuba ya kutosha, na upande kwa "proper spacing"itakayokupa mimea 20,000 hadi 22,000. Mfano kwa spacing ya 25cmx75cm plant population per acre 4000m2÷0.1875m2/plants=21,000plants.

Hii ndo idadi ya mimea inayopaswa kuota na kuzaa kwenye eneo la ekari moja.

Sasa shida wengi mnawaachia vibarua kuchimba mistari na kupanda mbegu. Matokeo yake wanachimba mistari na mashimo kwa umbali ili wamalize kazi haraka. Hapo ukihesabu mimea kwenye ekari unakuta kuna mimea elfu 15 au chini ya hapo. Ndio maana mkiona hizi takwimu hamuamini. Ukiwa serious haya mambo yanawezekana.
 
Shida yenu mnalima km babu zenu walivyolima ndio maana kila kitu hamuamini. We mtu unapanda ovyo ovyo,hauzingatii idadi ya mimea kwa ekari,shamba kubwaa mimea michache, hufanyi palizi kwa wakati,mbolea unaweka mara moja,toka babu hadi mjukuu shamba halijawahi rutubishwa kwa mbolea za asili kwanini usivune gunia 8 kwa ekari?

Hizo gunia 40-44 unazipata km shamba litakua na mimea 20,000 hadi 22,000. Sasa shida wengi mnawaachia vibarua kuchimba mistari na kupanda mbegu. Matokeo yake wanachimba mistari na mashimo mbalimbali ili wamalize haraka. Hapo ukihesabu mimea "per area"unakuta ekari moja ina mimea elfu 15 au chini ya hapo. Ndio maana mkiona hizi takwimu hamuamini.
Mavuno mengi pia watumie 9 seed hole, au bado wanapanda mbali mbali ndio maana wanashangaa.
 
Shida yenu mnalima km babu zenu walivyolima ndio maana kila kitu hamuamini. We mtu unapanda ovyo ovyo,hauzingatii idadi ya mimea kwa ekari,shamba kubwaa mimea michache, hufanyi palizi kwa wakati,mbolea unaweka mara moja,toka babu hadi mjukuu shamba halijawahi rutubishwa kwa mbolea za asili kwanini usivune gunia 8 kwa ekari?

Hizo gunia 40-44 unazipata km shamba litakua na rutuba ya kutosha, na upande kwa "proper spacing"itakayokupa mimea 20,000 hadi 22,000. Mfano kwa spacing ya 25cmx75cm plant population per acre 4000m2÷0.1875m2/plants=21,000plants.

Hii ndo idadi ya mimea inayopaswa kuota na kuzaa kwenye eneo la ekari moja.

Sasa shida wengi mnawaachia vibarua kuchimba mistari na kupanda mbegu. Matokeo yake wanachimba mistari na mashimo kwa umbali ili wamalize haraka. Hapo ukihesabu mimea ekari unakuta ina mimea elfu 15 au chini ya hapo. Ndio maana mkiona hizi takwimu hamuamini. Ukiwa serious haya mambo yanawezekana.
Asante kwa ushauri mkuu
 
DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni bora za kilimo.
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutosha bado hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave".
So hizi ndio mbegu bora za mahindi??
 
Angalizo: Mahali unapolima kama kuna joto kubwa kama la mkoa wa Pwani au Dar usipande karibu karibu kama ulivyo shauriwa na Kamgomoli na Depal hautapata mavuno mazuri utafeli kabisa. Nimejaribu mara kadhaa nimeon uhalisia. Nilipuuzia ushauri wa afisa kilimo wa eneo husika na wa wenyeji kuhusu joto.
 
Shida yenu mnalima km babu zenu walivyolima ndio maana kila kitu hamuamini. We mtu unapanda ovyo ovyo,hauzingatii idadi ya mimea kwa ekari,shamba kubwaa mimea michache, hufanyi palizi kwa wakati,mbolea unaweka mara moja,toka babu hadi mjukuu shamba halijawahi rutubishwa kwa mbolea za asili kwanini usivune gunia 8 kwa ekari?

Hizo gunia 40-44 unazipata km shamba litakua na rutuba ya kutosha, na upande kwa "proper spacing"itakayokupa mimea 20,000 hadi 22,000. Mfano kwa spacing ya 25cmx75cm plant population per acre 4000m2÷0.1875m2/plants=21,000plants.

Hii ndo idadi ya mimea inayopaswa kuota na kuzaa kwenye eneo la ekari moja.

Sasa shida wengi mnawaachia vibarua kuchimba mistari na kupanda mbegu. Matokeo yake wanachimba mistari na mashimo kwa umbali ili wamalize haraka. Hapo ukihesabu mimea ekari unakuta ina mimea elfu 15 au chini ya hapo. Ndio maana mkiona hizi takwimu hamuamini. Ukiwa serious haya mambo yanawezekana.
Miche 22,000 ili upate Tani ~40 Kila mche ukupe kilo~2....
 
I think changamoto kubwa kwenye kilimo kwa nchi yetu n kukosa wataalam. Maana waliopo wengi wao n wachumia tumbo na hata kama sio wachumia tumbo, sisi hatupendi kulipia ushauri n.k.

Hvyo tunaendelea kufanya the same thng over and over.

Mkuu Kamgomoli , kitu umesema personally ndo mara ya kwanza kuskia lakn imenifumbua macho ghafla. Kama hautojali ungeongeza nyama kidogo kwenye bandiko lako ili at least tupate mwangaza zaidi.

If only you are comfortable. No pressure.
 
I think changamoto kubwa kwenye kilimo kwa nchi yetu n kukosa wataalam. Maana waliopo wengi wao n wachumia tumbo na hata kama sio wachumia tumbo, sisi hatupendi kulipia ushauri n.k.

Hvyo tunaendelea kufanya the same thng over and over.

Mkuu @Kamgomoli , kitu umesema personally ndo mara ya kwanza kuskia lakn imenifumbua macho ghafla. Kama hautojali ungeongeza nyama kidogo kwenye bandiko lako ili at least tupate mwangaza zaidi.

If only you are comfortable. No pressure.
Sijajua unapenda nijazie wapi lakini ngoja niboreshe andiko langu lote kwa ujumla kuhsu kilimo cha Mahindi.

1.Kitu muhimu kabla ya kulima shamba hakikisha umelilisha chakula cha kutosha. Chakula cha shamba( udongo) ni samadi.Samadi huwaamsha "soil microbes" ambao wanaumuhimu mkubwa katika kuandaa na kutengeneza virutubisho vya udongo.Mbolea za viwandani hutumika km "supplement" tu na si za kuzitegemea 100%. Afya ya udongo haiboreki kwa kuweka mbolea za viwandani. Ni vema kwanza tukalijua hilo.

2. Kwa kawaida gari (tipa) lenye ujazo wa 4.5m3 linaweza kubeba trip 4 kwa eka moja na ikatosha. Uzuri wa samadi ya ngo'mbe inadumu kwenye udongo kwa mda mrefu. Kazi ya kumwaga samadi shambani ifanywe miezi ya kiangazi Mfano miezi ya August,September October hadi mwanzoni mwa Novemba. Kisha uisambaze kabla ya mvua kunyesha.

3. Ukisharutubisha shamba hapo ndo unaweza kuzitafuta hizo gunia 40. Sifa ingine ya samadi ni kutunza unyevu hasa miaka hii yenye tatizo la upungufu wa mvua.

4. Km utatumia vibarua wakati wa upandaji basi hakikisha umewasimamia vzri ili wachimbe mistari, mashimo na kupanda mbegu kwa usahihi.

5. Nafasi za upandaji wa mahindi inategemea na aina ya mbegu na ubora wa shamba. Km mbegu yako ni fupi unaweza kutumia "Spacing" ya kubananisha lakini hapo hapo ukiangalia ubora wa shamba. Km shamba ni dhaifu(halina rutuba ya kutosha) si vema kubananisha mimea itagombania chakula na kuwa dhaifa.
Hivyo Spacing zipo za aina nyingi. Utachagua mojawapo kutegemea na hizo factors juu nilizozieleza.
20cmx75
25cmx75
30cmx75-(Very common used).
60cmx75(two seeds per hole)
N.k

5. Palizi ya kwanza ifanyike wiki 2 hadi 3 toka mahindi kuoto kutegemea na kasi ya uotaji wa magugu. Hatua ya palizi ni muhimu sana kwani ukichelewa yataweza kuathiri ukuaji wa mahindi na vivyo hivyo kuathiri mavuno.

Nb: Mahindi ni mimea ambayo iko "sensitive" sana na magugu. Ukiyapalilia baada ya muda mfupi huanza kubadilika na kuwa mazuri na ukiyaacha kwenye msitu wa majani baada ya siku chache utakuta yameathirika. Hivyo ni vema shamba la mahindi liwe safi muda wote.
 
Sijajua unapenda nijazie wapi lakini ngoja niboreshe andiko langu lote kwa ujumla kuhsu kilimo cha Mahindi.

1.Kitu muhimu kabla ya kulima shamba hakikisha umelilisha chakula cha kutosha. Chakula cha shamba( udongo) ni samadi.Samadi huwaamsha "soil microbes" ambao wanaumuhimu mkubwa katika kuandaa na kutengeneza virutubisho vya udongo.Mbolea za viwandani hutumika km "supplement" tu na si za kuzitegemea 100%. Afya ya udongo haiboreki kwa kuweka mbolea za viwandani. Ni vema kwanza tukalijua hilo.

2. Kwa kawaida gari (tipa) lenye ujazo wa 4.5m3 linaweza kubeba trip 4 kwa eka moja na ikatosha. Uzuri wa samadi ya ngo'mbe inadumu kwenye udongo kwa mda mrefu. Kazi ya kumwaga samadi shambani ifanywe miezi ya kiangazi Mfano miezi ya August,September October hadi mwanzoni mwa Novemba. Kisha uisambaze kabla ya mvua kunyesha.

3.Ukisha rutubisha shamba hapo ndo unaweza kuzitafuta hizo gunia 40. Sifa ingine ya samadi ni kutunza unyevu hasa miaka hii yenye tatizo la upungufu wa mvua.

4. Km utatumia vibarua wakati wa upandaji basi hakikisha umewasimamia vzri ili wachimbe mistari, mashimo na kupanda mbegu kwa usahihi.

5. Nafasi za upandaji wa mahindi inategemea na aina ya mbegu na ubora wa shamba. Km mbegu yako ni fupi unaweza kutumia "Spacing" ya kubananisha lakini hapo hapo ukiangalia ubora wa shamba. Km shamba ni dhaifu(halina rutuba ya kutosha) si vema kubananisha mimea itagombania chakula na kuwa dhaifa.
Hivyo Spacing zipo za aina nyingi. Utachagua mojawapo kutegemea na hizo factors juu nilizozieleza.
20cmx75
25cmx75
30cmx75-(Very common used).
60cmx75(two seeds per hole)
N.k

5.Palizi ya kwanza ifanyike wiki 2 hadi 3 toka mahindi kuoto kutegemea na kasi ya uotaji wa magugu. Hatua ya palizi ni muhimu sana kwani ukichelewa yataweza kuathiri ukuaji wa mahindi na vivyo hivyo kuathiri mavuno.

Nb: Mahindi ni mimea ambayo iko "sensitive" sana na magugu. Ukiyapalilia baada ya muda mfupi huanza kubadilika na kuwa mazuri na ukiyaacha kwenye msitu wa majani baada ya siku chache utakuta yameathirika. Hivyo ni vema shamba la mahindi liwe safi muda wote.
Ahsante sana mkuu. Miaka yote mimi nilikua najua maximum unaeza pata per plot ni gunia 16 pekee. This time naona uwezekano wa kupata hzo zote hata kwa kujaribu eka moja kama shamba darasa maana ukusanyaji wa mbolea hua n changamoto.
 
Back
Top Bottom