Bangida
JF-Expert Member
- Mar 20, 2022
- 2,406
- 11,258
Kwa utaalam wako je kuna uwezekano wa kufanya maximization of output kwa zao kama maharage?Sijajua unapenda nijazie wapi lakini ngoja niboreshe andiko langu lote kwa ujumla kuhsu kilimo cha Mahindi.
1.Kitu muhimu kabla ya kulima shamba hakikisha umelilisha chakula cha kutosha. Chakula cha shamba( udongo) ni samadi.Samadi huwaamsha "soil microbes" ambao wanaumuhimu mkubwa katika kuandaa na kutengeneza virutubisho vya udongo.Mbolea za viwandani hutumika km "supplement" tu na si za kuzitegemea 100%. Afya ya udongo haiboreki kwa kuweka mbolea za viwandani. Ni vema kwanza tukalijua hilo.
2. Kwa kawaida gari (tipa) lenye ujazo wa 4.5m3 linaweza kubeba trip 4 kwa eka moja na ikatosha. Uzuri wa samadi ya ngo'mbe inadumu kwenye udongo kwa mda mrefu. Kazi ya kumwaga samadi shambani ifanywe miezi ya kiangazi Mfano miezi ya August,September October hadi mwanzoni mwa Novemba. Kisha uisambaze kabla ya mvua kunyesha.
3.Ukisha rutubisha shamba hapo ndo unaweza kuzitafuta hizo gunia 40. Sifa ingine ya samadi ni kutunza unyevu hasa miaka hii yenye tatizo la upungufu wa mvua.
4. Km utatumia vibarua wakati wa upandaji basi hakikisha umewasimamia vzri ili wachimbe mistari, mashimo na kupanda mbegu kwa usahihi.
5. Nafasi za upandaji wa mahindi inategemea na aina ya mbegu na ubora wa shamba. Km mbegu yako ni fupi unaweza kutumia "Spacing" ya kubananisha lakini hapo hapo ukiangalia ubora wa shamba. Km shamba ni dhaifu(halina rutuba ya kutosha) si vema kubananisha mimea itagombania chakula na kuwa dhaifa.
Hivyo Spacing zipo za aina nyingi. Utachagua mojawapo kutegemea na hizo factors juu nilizozieleza.
20cmx75
25cmx75
30cmx75-(Very common used).
60cmx75(two seeds per hole)
N.k
5.Palizi ya kwanza ifanyike wiki 2 hadi 3 toka mahindi kuoto kutegemea na kasi ya uotaji wa magugu. Hatua ya palizi ni muhimu sana kwani ukichelewa yataweza kuathiri ukuaji wa mahindi na vivyo hivyo kuathiri mavuno.
Nb: Mahindi ni mimea ambayo iko "sensitive" sana na magugu. Ukiyapalilia baada ya muda mfupi huanza kubadilika na kuwa mazuri na ukiyaacha kwenye msitu wa majani baada ya siku chache utakuta yameathirika. Hivyo ni vema shamba la mahindi liwe safi muda wote.