Shida yenu mnalima km babu zenu walivyolima ndio maana kila kitu hamuamini. We mtu unapanda ovyo ovyo, hauzingatii idadi ya mimea kwa ekari, shamba kubwaa mimea michache, hufanyi palizi kwa wakati, mbolea unaweka mara moja, toka babu hadi mjukuu shamba halijawahi rutubishwa kwa mbolea za asili kwanini usivune gunia 8 kwa ekari?
Hizo gunia 40-44 unazipata km shamba litakua na rutuba ya kutosha, na upande kwa "proper spacing"itakayokupa mimea 20,000 hadi 22,000. Mfano kwa spacing ya 25cmx75cm plant population per acre 4000m2÷0.1875m2/plants=21,000plants.
Hii ndo idadi ya mimea inayopaswa kuota na kuzaa kwenye eneo la ekari moja.
Sasa shida wengi mnawaachia vibarua kuchimba mistari na kupanda mbegu. Matokeo yake wanachimba mistari na mashimo kwa umbali ili wamalize kazi haraka. Hapo ukihesabu mimea kwenye ekari unakuta kuna mimea elfu 15 au chini ya hapo. Ndio maana mkiona hizi takwimu hamuamini. Ukiwa serious haya mambo yanawezekana.