duh mie na kupika vitu viwili tofauti anyway labda nijifunze ukubwani nadhani siku hiyo wife anaweza kuzirai kwa mshangao maana hata pa kuwashia jiko sipajuiMkuu Funzadume sio lazima ukate vitunguu hata kugeuzakeuza vilivyopo jikoni ukimsaidia kukarangiza sio mbaya, HG nae anatakiwa apumzike akapunguze uzito nje jamani
Inabidi uache kufanya mbele za watoto. kipindi cha likizo watafutie watoto na mayaya wao likizo kwa bibi wakakae huko hata wiki mbili nyie huku mnajinafasi
Kutekenyana sawa lakini kupakatana na ku busiana je............kwenda kuoga pamoja?
...No wonder wengine wakilalamikiwa "siku hizi hunijali wala hunifanyii yale ulokuwa unanifanyia zamani" wanabakia kushangaa!
Yaani usubirie mpaka mid-term au Annual leave ndio uanze 'kuibia' kwa mkeo/mumeo?
eti kwakuwa tu watoto hawapo?
aaarrggh!
je mfano mkeo bado anaonekana vizuri na kuvutia?Ingawa maadili yamepotea siku hizi kwa watoto wetu ila haiwezi kuzuia wazazi kufanya mambo waliyokuwa wakifanya zamani,tatizo hapa ni kuwa kwa wanandoa ambao wamepata watoto hujisahau kabisa na mambo ya mapenzi na wakati mwingine huwa ile hamu ya kufanyiana mambo ya kimahaba kama wakati wa uchumba inakuwa imekwisha.Maisha kabla ya watoto na baada ya watoto ni tofauti sana hasa katika familia zetu za kiafrika,kinamama hujisahau sana hasa kimuonekano,utamkuta yupo yupo tu kiasi kwamba hata havutii kumbusu na muda mwingi anautumia kwa watoto badala ya mumewe,na kwa kina baba utakuta wakati mkewe ni mjamzito yeye keshatafuta nyumba ndogo siku nyingi,mpaka watoto wanakuwa anakuwa amekwishapoteza ile hamu ya vionjo vya kimahaba na mkewe ndio maana inakuwa ngumu sana kuona mambo haya baada ya ndoa.
hiyo ya kupika pamoja mie siwezi yaani katika vitu ambavyo sipendi duniani ni kupika kuna siku nilijaribu vitunguu vikaniingia machoni toka siku ile imepita miaka zaidi ya 15 sijaingia jikoni na nimeajiri house girl kumsaidia wife kwenye hiyo sector so siwezi kuingilia kabisa
Hahahahahahahaha Mbu inaelekea hulali mbali na nyeti zako ukishtuka tu unataka uzione kama bado zipo lol! Haya Mkuu. Umesikia kuna kifaa kimoja cha miaka 18 kule kwetu. Wenger kawaambia UK wakidake haraka katika National Team kabla ya Ghana kufanya hivyo maana kina Udc wa nchi hizo mbele na Wenger anadai ni moto wa kuotea mbali..
Inabidi uwe makini sana na watoto maana wanaweza kuiga mambo unayofanya.Ila kumbusu,kuoga,na mambo mengine yasiyo ya kimahaba yanaweza ka ila kwa yale yanayozidi kwa kweli tuyafanye faragha zaidi maana tutawaharibu watoto.
Ingawa maadili yamepotea siku hizi kwa watoto wetu ila haiwezi kuzuia wazazi kufanya mambo waliyokuwa wakifanya zamani,tatizo hapa ni kuwa kwa wanandoa ambao wamepata watoto hujisahau kabisa na mambo ya mapenzi na wakati mwingine huwa ile hamu ya kufanyiana mambo ya kimahaba kama wakati wa uchumba inakuwa imekwisha.Maisha kabla ya watoto na baada ya watoto ni tofauti sana hasa katika familia zetu za kiafrika,kinamama hujisahau sana hasa kimuonekano,utamkuta yupo yupo tu kiasi kwamba hata havutii kumbusu na muda mwingi anautumia kwa watoto badala ya mumewe,na kwa kina baba utakuta wakati mkewe ni mjamzito yeye keshatafuta nyumba ndogo siku nyingi,mpaka watoto wanakuwa anakuwa amekwishapoteza ile hamu ya vionjo vya kimahaba na mkewe ndio maana inakuwa ngumu sana kuona mambo haya baada ya ndoa.
Kwa wale wenzangu na mie wanandoa kuna ile hali kipindi cha uchumba na kipindi cha ndoa kabla ya kupata watoto na kuwa na wafanyakazi ndani ya nyumba kuna zile za kukumbatiana au kupigana mabusu, kulaliana kwenye makochi mkiangalia TV na vimbwanga vingine vya kimahaba vinavyofanyika nje ya chumba mfano sebuleni, jikoni na sehemu nyingine.
Je mkipata watoto inabidi vitu vile mviache na kuvifanya chumbani tu ambako kwa kawaida hamshindi huko muda mrefu au viendelee tu mbele ya watoto?
...halafu, kwani hii topic ni ngumu kivile? mbona wachangiaji kina mamaa siwaoni humu?
In no particular order; Nyamayao, Mwanajamii1, bht, Jocelyne1, 1stLady, BJ, WoS etc etc...
mpendwe vipi nasi tuelewe?..he he he...kaazzzi kwelikweli hizi ndoa.
Wame 'Myuti' aisee!
ngoja nikupe deal achana na kufua mtu wangu kuna mashine za wash and dry pale Mlimani City zinauzwa bei chee kama laki 4 hivi na wala hazili umeme ila maji tu na sabuni lakini ni bomba wala huangaiki kihivyo mie kufua toka nimepata zile mashine (tena kwa bei ya promesheni) sio issue tena kwanguUwe unafua naye! Mie kufua ndo shughuli
Mkuu kama unamsaidizi wa ndani, hicho ni kibano! nikuzuga nakuwaambia hasa siku za weekend waende bucha ili ujinafasi. Vinginevyo, itaonekana hutoi dozi halisi!hapo muwe hamna housigelo au housiboi maana nao utakuta baada ya kazi anashindilia tamthilia mpk saa sita usiku na vitoto vingine havilali mpaka viangalie kina Marichuy na Juan Miguel sasa hapo mtafanya nn zaidi ya kusubiri wakati wa kulala
umeongea point sana dark city wa mazimbu morogoroKila kitu kinatakiwa kufanyika kwa mahesabu baada ya kupata watoto. Life will never be the same after the number has increased from two of you to three etc. Kwa hiyo inatakiwa busara ili muweze kufanya baadhi ya vitu mbele yao na vingine chumbani. Pia ni muhimu kuweka utaratibu wa watoto kulala mapema. Kwangu watoto mwisho ni saa 4. Wanatakiwa kuwa kitandani kuanzia saa 3.30. Hivyo vitu mnavyofanya mbele ya watoto ni muhimu sana ili kuwajenga katika hali ya kupendana. Hata wakiwa na wake au waume zao wajue ni marafiki zao ni siyo watumishi au maboss! Vitu vinavyoelekea kwenye ngono zaidi ni marufuku mbele ya watoto, vinginevyo kesho au kesho kutwa utaitwa shuleni kusikiliza kesi ya mwanao akitoa demo mbele ya wenzake.
I LIKE TTV zetu zina haribu watoto wetu huu utandawazi umewatandaa vibaya.
Kuna vitu ambavyo mnaweza kuviendeleza kama kuoga pamoja, kupigana mabusu ( sio denda) mkatumia glass moja kunywea kama ni wine, juice nk wakati mnaangalia TV mkakaa kochi moja kkuangalia tv unaweza hata kumwekea mwenzi wako miguu wakati wa kuangalia TV wakati mwingine hata kupika pamoja pia mnaweza pika siku mama yuko jikoni sio vibaya baba nae akawa nae jikoni wakapika pamoja