Ingawa maadili yamepotea siku hizi kwa watoto wetu ila haiwezi kuzuia wazazi kufanya mambo waliyokuwa wakifanya zamani,tatizo hapa ni kuwa kwa wanandoa ambao wamepata watoto hujisahau kabisa na mambo ya mapenzi na wakati mwingine huwa ile hamu ya kufanyiana mambo ya kimahaba kama wakati wa uchumba inakuwa imekwisha.Maisha kabla ya watoto na baada ya watoto ni tofauti sana hasa katika familia zetu za kiafrika,kinamama hujisahau sana hasa kimuonekano,utamkuta yupo yupo tu kiasi kwamba hata havutii kumbusu na muda mwingi anautumia kwa watoto badala ya mumewe,na kwa kina baba utakuta wakati mkewe ni mjamzito yeye keshatafuta nyumba ndogo siku nyingi,mpaka watoto wanakuwa anakuwa amekwishapoteza ile hamu ya vionjo vya kimahaba na mkewe ndio maana inakuwa ngumu sana kuona mambo haya baada ya ndoa.