Mbeligiji Adel Amrouche (58) ateuliwa kuwa kocha Mpya Taifa Stars

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linamtangaza Adel Amrouche (58) kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Kocha Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa katika ukanda Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.

Amewahi kuwa Kocha Bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa na kuipa Kenya, Harambee Stars ubingwa wa Cecafa Challenge na kabla alifika nusu fainali mara mbili akiwa na Burundi.

Akiwa na Harambee Stars aliweka rekodi ya kucheza michezo 20 bila kupoteza.

Kocha Amrouche amewahi pia kuzinoa timu za taifa za Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen kwa nyakati tofauti.

Akinoa DC Motema Pembe aliiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho akiwa ameipa mara mbili ubingwa wa DR Congo na DRC Super Cup.

Uzoefu mwingine kwa klabu, amezifundisha RC Kouba, USM Alger, alizowahi kuzichezea na MC Algiers, zote za Algeria.

Aidha, Kocha Adel ni mkufunzi wa walimu wa Pro Licence wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) akizalisha makocha wengi bora barani Afrika na ana uzoefu mkubwa katika soka la vijana, kazi aliyoifanya kwa zaidi ya miaka 10 chini Algeria na Ubelgiji

Kocha Amrouche anayezungumza lugha za Kiarabu, Kifaransa, Kingereza na Kiswahili, kwa nyakati tofauti, amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Michezo katika klabu za Ubelgiji na Ukraine.

Kocha mwenye Uefa Pro Licence na Shahada ya Uzamili katika kuwasoma watu na Utimamu (Mas- ters in Ergonomics in Physical Activity) Amrouche amekuwa akifanya kazi za ukufunzi pia kwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kuzalisha walimu wa soka. Katika wakati wote wa Mkataba wake Amrouche atalipwa mshahara na Serikali.

94788A34-225D-427B-BEA7-FF252758B0C9.jpeg
 
Huyu Kocha ana CV nzito sana, ngoja tusubiri kuona Uwanjani

Nadhani TFF Wamefuata ushauri wa Mzee Mpili, TFF kama wanataka Kocha wamtafute kwenye dugo (Google) lakini si Nabi.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemtangaza Adel Amrouche kuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars.

Amrouche ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria amewahi kuzinoa timu mbalimbali kama Harambee Stars (timu ya Taifa ya Kenya) ambayo aliipa ushindi wa Cecafa 2013. Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen.

Kwa upande wa klabu amezinoa USM Alger, RC Kouba na MC Algiers.
 
Kusema kocha mbelgiji then hajachezea klabu yeyote ya ulaya ujue kocha wa mchongo huyo

Cv inasema amewahi kuwa mkurugenzi wa ufundi vilabu vya ulaya ila hajitajwa badala yake vimetajwa vya africa tu

Cv ya mchongo
 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linamtangaza Adel Amrouche (58) kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Kocha Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa katika ukanda Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.

Amewahi kuwa Kocha Bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa na kuipa Kenya, Harambee Stars ubingwa wa Cecafa Challenge na kabla alifika nusu fainali mara mbili akiwa na Burundi.

Akiwa na Harambee Stars aliweka rekodi ya kucheza michezo 20 bila kupoteza.

Kocha Amrouche amewahi pia kuzinoa timu za taifa za Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen kwa nyakati tofauti.

Akinoa DC Motema Pembe aliiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho akiwa ameipa mara mbili ubingwa wa DR Congo na DRC Super Cup.

Uzoefu mwingine kwa klabu, amezifundisha RC Kouba, USM Alger, alizowahi kuzichezea na MC Algiers, zote za Algeria.

Aidha, Kocha Adel ni mkufunzi wa walimu wa Pro Licence wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) akizalisha makocha wengi bora barani Afrika na ana uzoefu mkubwa katika soka la vijana, kazi aliyoifanya kwa zaidi ya miaka 10 chini Algeria na Ubelgiji

Kocha Amrouche anayezungumza lugha za Kiarabu, Kifaransa, Kingereza na Kiswahili, kwa nyakati tofauti, amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Michezo katika klabu za Ubelgiji na Ukraine.

Kocha mwenye Uefa Pro Licence na Shahada ya Uzamili katika kuwasoma watu na Utimamu (Mas- ters in Ergonomics in Physical Activity) Amrouche amekuwa akifanya kazi za ukufunzi pia kwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kuzalisha walimu wa soka. Katika wakati wote wa Mkataba wake Amrouche atalipwa mshahara na Serikali.

View attachment 2536776
Kwa aina ya timu yetu na wachezaji wake, sitegemei maajabu yoyote yale kutoka kwake.
 
Hizo sifa za wasifu wake hazina maana yote kwa sisi watanzania tunaotaka sasa timu yetu apewe kocha mtanzania (mzawa).

Hiyo nafasi alipaswa apewe Juma Mgunda, lakini wamembania tu kisa ni mbongo.
 
Timu ya taifa apewe mzawa
Hata akipewa kati ya wanaoaminiwa na wengi yaani Yesu au Mtume Mudd bado hatutapiga hatua kwenda mbele. Mpira na michezo mingine inahitaji maandalizi thabiti na endelevu siyo zima moto.

Maximo alikuwa Mwl mzuri na mara zote alitwambia ukweli lkn kwakuwa cc ni kichwa cha mwendawazimu tukamuona kuwa anatuchelewesha. Tunajifanya tuna nia lkn hatuna malengo ya muda mrefu. Acha waje waendelee kuchukua kodi zetu kwakuwa hazina kazi.
 
Back
Top Bottom