Mbeto ashauri wazanzibari kuupuza kauli za kiongozi wa AAF Said Soud

Mbeto ashauri wazanzibari kuupuza kauli za kiongozi wa AAF Said Soud

Thabit Madai

Member
Joined
Oct 8, 2024
Posts
54
Reaction score
140
IMG-20250125-WA0021.jpg




Chama Cha Mapinduzi kimewaomba wananchi wa Zanzibar kumsikiliza, kumtafakari,kumtazama hatimaye kumpuuza Mwenyekiti wa AAFP Said Soud Said aliyedai zanzibar haina maendeleo yoyote kwa miaka mitano iliopita .

Pia CCM kimeiomba Ofisi ya Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar kukitazama chama hicho ikiwa bado kinakidhi vigezo vya kuendelea kubaki kuwa chama cha Siasa.


Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ofisini kwake kisiwandui kufuatia matamshi ya chuki yaliotamkwa na Mwenyekiti wa AAFP.

Mbeto alisema shutuma za Said hazionyeshi ukomavu wenye dhima ya kuendeleza umoja wa kitaifa , upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania .

Alisema ametoa shutuma ambazo hazina ushahidi ikiwemo kukosa busara na hekima zinazomuonyesha kiwango cha kiongozi wa chama siasa kilichosajiliwa kisheria , chenye katiba na wanachama kwa mujibu wa katiba yake.

'AAFP si kwamba kimekuwa kikishabikia shari, chuki na kupandikiza hasama. Pia sina hakika kama kina wanachama wanaofikia mia Tanzania nzima . AAFP siku zote anayeonekana ni Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake "Alisema Mbeto


Alisema kinachosikitisha ni kumsikia Mwenyekiti wake akidai tokea Rais Dk Hussein Ali Mwinyi ashike madaraka, Zanzibar haijapata maendeleo huku baadhi ya watu wake wanalala na njaa ,wengine wakipoteza maisha.

"Hakuna mwananchi aliyekufa kwa njaa unguja au Pemba.Said na AAFP tunataka watoe ushahidi utakaoithibitishia dunia. Said ataje ni mranzania yupi aliyrkufa kwa njaa , lini na mahali gani" Alisema Mbeto

Aidha akizungumzia kuhusu sheria Namba 4 ya Mwaka 2018 kuhusu kura ya mapema, Mbeto alisema Mwenyekiti huyo wakati akiwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alikuwa mjumbe mmojawapo aliyepiitisha sheria hiyo.


Alisema hadhani kama chama hicho huendesha shughuli zake za kisiasa kwa mujibu wa katiba ikiwemo kuitisha vikao ,pia alidai hajui kama hakijapoteza sifa ya kuitwa chama cha siasa ikiwa hakina wanachama .

"Kwa muktadha huo AAFP si kwamba hakina haki ya kuwasemea wanachama wake lakini pia kinakosa uhalali wa kuwasemea watanzania. Ziko wapi ofisi za AAFP .Kiache kufanya udalali wa kisiasa kiendelee na kazi za kisiasa " Alieleza

Hata hivyo Mbeto ameyaita matamshi yaliotamkwa na Mwenyekiti wa AAFP ,licha ya kukosa mizania , si chama cha kizalendo kwa kukosa nidhamu na maadili ya uongozi.

"Tunaiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa iliopo zanzibar kukifuatilia kwa karibu chama hiki . AAFP kinaonekana kukiuka Sheria Namba 5 ya Mwaka 1992 kwa kutoheshimu umoja na utulivu " Alisisitiza Mbeto
 
Back
Top Bottom