Mbeya: Ajifungia kwenye nyumba yeye na mkewe kisha kuchoma nyumba moto, kisa wivu wa mapenzi

Mbeya: Ajifungia kwenye nyumba yeye na mkewe kisha kuchoma nyumba moto, kisa wivu wa mapenzi

Mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Nyigamba Kata ya Itezi mkoani MBEYA aliyefahamika kwa jina la Hamis Pius amejiua kwa kujichoma moto kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

mashariki Mkoa wa Mbeya amejiondoa uhai wake kwa kujichoma Mto aliouwasha kwa makusudi ,akiwa amefanya maandalizi kwa kununua mafuta ya petrol na kumuita mkewe chumbani Ili wafe wote sababu ikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza kuwa marehemu alifanya tukio Hilo kwa kudhamiria ili kujiondoa uhai yeye na familia yake. Marehemu anadaiwa kuwasha moto huo kwa makusudi baada ya kumwaga petroli akiwa ndani pamoja na familia yake, lakini taarifa ya jeshi la Polisi inaeleza kuwa mtoto wa marehemu mwenye miaka 20 ndiye aliyemuokoa Mama yake kwenye moto huo lakini walitoka wakiwa na majeraha na kuwahishwa hospitali kwa matibabu.

 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya kuoa.
 
Tumeingia kwenye age ambayo mwanamke anataka kushindana na mwanaume kwenye kila nyanja
Ndomana majumbani,kwenye ndoa ni vurugu mechi

Ova
 
View attachment 2549166
Mtoto wa marehemu akiwa Hospitalini akiendelea na matibabu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni, misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Aidha tumeendelea kupata mafanikio kwa kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali na kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin E. Kuzaga amesema Mnamo tarehe 08.03.2023 majira ya saa 04:00 usiku huko maeneo ya Nyigamba, Mtaa wa Itezi, Jijini Mbeya, mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la HAMIS PIUS [41] Dereva, Mkazi wa Nyigamba alifariki dunia kwa kuungua moto baada ya kujifungia ndani ya chumba anacholala na mke wake aitwaye REBELIA MAKOSO [38] Mkazi wa Nyigamba kisha kumwaga mafuta ya Petroli na kuwasha moto.

Wakati wa tukio hilo, mke wa marehemu alipiga kelele kuomba msaada kwa mtoto wake aitwaye MKESHILISI HAMIS [21] ambaye alikuwa chumba kingine ambaye alikwenda kutoa msaada kwa kupiga teke mlango wa chumba na kisha kumuokoa mama yake lakini baba yake alikataa kutoka ndani na kupelekea kuungua hadi kupoteza maisha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Majeruhi ambao ni mke na mtoto wa marehemu wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi kutokana na majeraha ya moto waliyoyapata mwilini.
View attachment 2549167
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin E. Kuzaga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi. Aidha tunatoa wito kwa jamii kutatua migogoro yao ya kifamilia na ndoa kwa kukaa meza moja ya usuluhishi badala ya kuchukua maamuzi magumu kama hayo.
CHANZO kwanini haisemwi ni KUKOSEKANA UAMINIFU KTK NDOA/ USALITI KWA WANANDOA!!!na iwekwe wazi WITO: wanandoa waache UZINZI na uasherati na UKAHABA/PROSTITUTION kupunguza haya mauaji yanayotakana na USALITI.
 
Back
Top Bottom