KERO Mbeya: Baadhi ya Mitaa ya Jiji la Mbeya ni michafu, tunakaribisha Milipuko ya Magonjwa

KERO Mbeya: Baadhi ya Mitaa ya Jiji la Mbeya ni michafu, tunakaribisha Milipuko ya Magonjwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Leo katika pitapita zangu kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya nimejionea namna ambavyo Jiji hili lilivyo chafu.

Viroba vya takataka vimerundikwa kila mahali katika mitaa ya Jiji hili.

Wenye mamlaka ya kukusanya taka nao ni kama hawaoni namna ambavyo Jiji limetapakaa uchafu.

Pichani ni mfano tu wa hali ilivyo, hapa ni Mitaa ya Kabwe ambapo ni katikati ya Jiji. Hii sio sawa hata kidogo.

Pia soma: DOKEZO - Mbeya: Wafanyakazi wa Dampo la Nsalaga wageuka wafanyabiashara wa bidhaa zinazotupwa hapo

Tunaelekea kipindi cha masika chondechonde ndugu zangu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya oneni hili la sivyo tutapata magonjwa ya mlipuko.

DSC_0136.JPG
DSC_0137.JPG
 
Mkuu uwe unatembea angalau hata hata Zimbabwe tu hapo,ukiacha dar angalau kidogo yanayoitwa majiji ni vijiji tu vikubwa vyenye mpangilio mbaya.

Ushawahi kuishi Mbeya?

Unashangaza endapo unaona mji wa Mbeya kuwa nao ni jiji...

Just to let you know, nimefika majiji haya duniani Jozi, Addis Ababa. Nairobi, Dallas, St Louis, Jefferson City, Tulsa, Kansas City, Little Rock, Hong Kong, Beijing, Guangzhou, Shenzhen, Wuhan, Dubai, Doha etc....kwa hiyo nina uelewa mpana kuhusu majiji
 
Sio jiji Tu hata watu wa mbeya kiasili ni wachafu, kujenga wamejenga hovyohovyo bila mpangilio, Kilimanjaro hadi mabibi vijijini husafisha mazingira kuzunguka nyumba kila asubuhi na kupanda Maua na bustani nzuri mbeya Hilo halipo , wako rafu hata mitaa yao haijapangika kwa barabara kama hata makambako, mbinga, babati, kahama, ifakara , mbeya wanajua kujirundika kama viroba vya takataka sehemu moja , msiba unatokea inabidi aombe kwa jirani,
 
Kwa ufupi mbeya haikutakiwa kua jiji huwezi kuita green city wakati hakuna ukijani kupanda miti Bora hata pembezoni mwa barabara hawawezi watu wa ajabu Sana mbeya
 
𝗡𝗮 𝗵𝗲𝗹𝗮 𝘇𝗮 𝘁𝗮𝗸𝗮𝘁𝗮𝗸𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗸𝘂𝘀𝗮𝗻𝘆𝗮 ?
 
Ushawahi kuishi Mbeya?

Unashangaza endapo unaona mji wa Mbeya kuwa nao ni jiji...

Just to let you know, nimefika majiji haya duniani Jozi, Addis Ababa. Nairobi, Dallas, St Louis, Jefferson City, Tulsa, Kansas City, Little Rock, Hong Kong, Beijing, Guangzhou, Shenzhen, Wuhan, Dubai, Doha etc....kwa hiyo nina uelewa mpana kuhusu majiji
Sijui anasema mbeya ipi ya uyole? Sai , ilomba, itua, veta, nzovwe, iyunga, forest ? Kidogo iwambi walijipanga, iyunga huko , kalobe, must, kote kubovu mbeya wanajua kuchoma nyama zao kishamba, na kujaza mafuta kwenye michips yao , kupika tu hawajui wao wanaloweka tu basi,
Kile ni kijiji chenye watu wengi ambacho haijapangika
 
Back
Top Bottom