Mbeya: Bajaji yajaza abiria kupita kiasi hadi dereva kuendeshea akiwa ametoa kiuno na miguu nje

elninyo

Member
Joined
Aug 29, 2026
Posts
8
Reaction score
11

Ndugu wanajamii na mamlaka husika,

Huu ni uendeshaji hatari sana wa chombo cha moto na ni jambo ambalo halipaswi kuachwa liendelee kuwa kawaida.

Kama inavyoonekana kwenye video, dereva wa bajaji hii amejaza abiria kupita kiasi hadi amekosa kabisa nafasi ya kawaida ya kukaa. Ili kuweza kuendesha, amelazimika kutoa sehemu ya mwili wake nje na wakati mwingine hata mguu nje huku chombo kikiwa kwenye mwendo. Hii ni hatari kwa dereva mwenyewe, abiria, pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Hata hivyo, ni muhimu pia kuangalia mazingira yaliyosababisha hali hii. Kwa kiasi kikubwa, hali ya leo imechangiwa na mgomo wa daladala Mbeya, ambao umewalazimu abiria wengi kuhamia kwenye bajaji na kusababisha msongamano mkubwa na usafiri wa bajaji kulemewa. Kwa hiyo, mazingira ya leo yalikuwa tofauti na siku za kawaida.

Pamoja na hilo, mgomo hauondoi kabisa wajibu wa dereva. Uamuzi wa kubeba abiria kupita uwezo wa bajaji na kuendesha akiwa katika hali hiyo ni hatari na dereva anapaswa kutambua madhara yanayoweza kutokea. Tatizo ni kwamba, kwa bahati mbaya, aina hii ya uendeshaji imekuwa ikionekana pia siku nyingine, hasa nyakati za asubuhi na jioni wakati wa misongamano mikubwa.

Lengo la kuleta video hii hapa jukwaani siyo kutaka dereva huyu apewe adhabu kali iliyopitiliza au kupoteza kabisa chanzo chake cha riziki. Ni muhimu mamlaka zitazame suala hili kwa mtazamo mpana, kwa sababu mara nyingi madereva hawa wanafanya kazi katika mazingira yenye presha kubwa ya kutafuta hesabu za kila siku.

Rai yangu kwa mamlaka husika, ikiwemo Kikosi cha Usalama Barabarani na LATRA, ni:

1. Kutatua changamoto ya usafiri wa daladala

Mgomo wa daladala unapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa usafiri wa umma na kuwalazimisha abiria wengi kutegemea bajaji. Hali hii inapozidi, huongeza msongamano na kuwaweka madereva wa bajaji kwenye presha kubwa ya kubeba abiria wengi zaidi. Ni muhimu chanzo cha tatizo la usafiri kishughulikiwe ili kupunguza mzigo huu.

2. Kutoa elimu na tahadhari kwa madereva

Dereva huyu na wengine wenye tabia kama hii wapewe elimu na tahadhari kuhusu madhara ya kubeba abiria kupita uwezo wa chombo. Onyo la wazi litolewe kwa madereva wote kwamba hata katika mazingira ya msongamano au upungufu wa usafiri, usalama haupaswi kuachwa nyuma.

3. Hatua iwe ya kumrekebisha, siyo kumwangamiza

Ikiwa mamlaka itaona ni lazima hatua ichukuliwe dhidi ya dereva huyu, naomba izingatie adhabu inayolingana na kosa, kama vile faini na elimu ya usalama barabarani, badala ya hatua inayoweza kumkatisha kabisa riziki. Hii siyo kumtetea dereva kwa alichofanya, bali ni kuomba hatua inayomfundisha na kurekebisha tabia bila kumwangamiza.

4. Kuangalia presha ya hesabu kwa madereva

Madereva wengi wanaoendesha bajaji kwa mikataba wanakuwa na presha kubwa ya kufikisha hesabu za kila siku. Presha hii inaweza kuwafanya baadhi yao kuchukua risks barabarani ili kuongeza mapato. Ni muhimu mamlaka na wahusika katika sekta hii kuangalia kama kuna namna ya kuweka utaratibu wa mikataba unaopunguza presha hiyo bila kuathiri usalama.

5. Kudhibiti uendeshaji wa bajaji na madereva wasio rasmi

Kuwe na utaratibu mzuri wa kuhakikisha bajaji haiendeshwi na mtu mwingine kiholela wakati dereva wake amechoka au anahitaji kupumzika. Kuna maeneo, hasa kwenye vituo vya kupigia debe, ambapo dereva anaweza kumpa mtu mwingine bajaji aendeshe kwa muda, hata kama siyo dereva rasmi wa chombo hicho. Hali hii inaweza kuongeza hatari kwa sababu dereva mwingine anaweza kuwa hana uzoefu, hana taarifa sahihi za chombo au akawa anakimbizana na muda.

Ni matumaini yangu kuwa mamlaka zitaangalia suala hili kwa mtazamo wa usalama lakini pia kwa kuzingatia mazingira halisi ambayo madereva na abiria wanakutana nayo.

Dereva huyu amekosea na anapaswa kuwajibika kwa kiwango kinachostahili, lakini pia tusisahau kwamba mazingira ya usafiri, mgomo wa daladala, msongamano na presha za kiuchumi vina mchango katika kuzalisha tabia hizi.

Credit: alierekodi na kushea video hio na kuisambaza kwenye magroup
 
Ndugu wana jamii na mamlaka husika,

Huu ni uendeshaji hatari sana wa chombo cha moto.

Kama inavyoonekana kwenye video hii niliyoiambatisha, dereva wa bajaji hii amejaza abiria kupita kiasi hadi amekosa kabisa nafasi (siti) ya kukaa.

Ili kuweza kuendesha, amelazimika kutoa kiuno chake nje na muda mwingine anatoa hadi mguu nje huku chombo kikiwa kwenye mwendo. Huu ni uendeshaji hatari unaohatarisha maisha yake yeye mwenyewe, abiria waliomo ndani, na watumiaji wengine wa barabara.

Hata hivyo, lengo la kuleta video hii hapa jukwaani siyo kutaka dereva huyu apewe adhabu kali sana au kufungiwa maisha, kwani tunaelewa huku mitaani hii imekuwa ni tabia ya kuigana na wengi wanafanya hivi kwa mazoea mabaya tu.

Rai yangu kwa mamlaka husika (kama vile Kikosi cha Usalama Barabarani na LATRA) zitakapochukua hatua:

1. Kutoa Elimu na Tahadhari: Dereva huyu na wengine mitaani wapewe elimu ya usalama kwanza. Vyombo vinavyohusika vitoe onyo rasmi na la wazi kwa madereva wote kuhusu hatari ya tabia hii.

2. Adhabu ya Faini pekee: Badala ya kumpotezea kabisa riziki yake huyu kijana, nawaombeni msimpe adhabu kali iliyopitiliza. Naomba apigwe faini iwe fundisho kwake. Binafsi nitajutia sana kushirikisha video hii hapa, na nitakosa kabisa ari ya kuweka video nyingine nikisikia kijana huyu kapewa adhabu kali iliyopitiliza na kukandamizwa.

3. Kuona namna ya kuwapunguzia presha madereva kwenye hesabu: Dereva huyu na wengine wanaopewa bajaji kwa mikataba wana presha kubwa sana ya kufikia hesabu za mabosi wao kila siku. Hali hii inawafanya wachukue hatari (risks) kubwa kama hizi barabarani ili kupata pesa. Itapendeza kuona jinsi gani gharama au utaratibu mpya wa mikataba unavyoweza kuwekwa ili kupunguza presha hii kwa vijana.

4.kuwe na utaratibu wa kuzuia madereva kutoa bajaji zao wanapochoka, kuna muda hasa eneo la kupigia debe, dereva anaweza kumpa bajaji mtu mwengine aendeshe hata mpiga debe na hata huyo dereva yawezekana sio dereva rasmi wa hiyo bajaji kaazimwa tu kwa muda mchache hivyo anakimbizana na muda

Ni matumaini yangu kuwa hatua hizi zitasaidia kunyoosha tabia za madereva wetu bila kuwaharibia maisha yao kabisa, bali kuwajenga kuwa watumiaji wazuri wa barabara.
Wenu katika ujenzi wa taifa salama.
ok.🐒
 
Mjomba hiyo picha/video iko wapi?
Kama vipi toa hela tukusaidie.
 
Maelezo marefuuuuuu no fotoglafu no video
 
Umeiweka vema sana hii habari. Nawewe ndugu elninyo usitutishe sana hadi tumekuwekea bajeti ya bilioni za fedha.

Usije tafadhari.
 
Watu wa musoma wote hawana plug.
1.Waliwahi kugombania bagia
2.Walipoteza uhai wa mtu kisa laki 3.
3.wanapanda hadi 10 kwenye bajaj 1.
4.Matapeli Xmtume.

Niishie hapa
 
View attachment 3665478

Ndugu wana jamii na mamlaka husika,

Huu ni uendeshaji hatari sana wa chombo cha moto.

Kama inavyoonekana kwenye video hii niliyoiambatisha, dereva wa bajaji hii amejaza abiria kupita kiasi hadi amekosa kabisa nafasi (siti) ya kukaa.

Ili kuweza kuendesha, amelazimika kutoa kiuno chake nje na muda mwingine anatoa hadi mguu nje huku chombo kikiwa kwenye mwendo. Huu ni uendeshaji hatari unaohatarisha maisha yake yeye mwenyewe, abiria waliomo ndani, na watumiaji wengine wa barabara.

Hata hivyo, lengo la kuleta video hii hapa jukwaani siyo kutaka dereva huyu apewe adhabu kali sana au kufungiwa maisha, kwani tunaelewa huku mitaani hii imekuwa ni tabia ya kuigana na wengi wanafanya hivi kwa mazoea mabaya tu.

Rai yangu kwa mamlaka husika (kama vile Kikosi cha Usalama Barabarani na LATRA) zitakapochukua hatua:

1. Kutoa Elimu na Tahadhari: Dereva huyu na wengine mitaani wapewe elimu ya usalama kwanza. Vyombo vinavyohusika vitoe onyo rasmi na la wazi kwa madereva wote kuhusu hatari ya tabia hii.

2. Adhabu ya Faini pekee: Badala ya kumpotezea kabisa riziki yake huyu kijana, nawaombeni msimpe adhabu kali iliyopitiliza. Naomba apigwe faini iwe fundisho kwake. Binafsi nitajutia sana kushirikisha video hii hapa, na nitakosa kabisa ari ya kuweka video nyingine nikisikia kijana huyu kapewa adhabu kali iliyopitiliza na kukandamizwa.

3. Kuona namna ya kuwapunguzia presha madereva kwenye hesabu: Dereva huyu na wengine wanaopewa bajaji kwa mikataba wana presha kubwa sana ya kufikia hesabu za mabosi wao kila siku. Hali hii inawafanya wachukue hatari (risks) kubwa kama hizi barabarani ili kupata pesa. Itapendeza kuona jinsi gani gharama au utaratibu mpya wa mikataba unavyoweza kuwekwa ili kupunguza presha hii kwa vijana.

4.kuwe na utaratibu wa kuzuia madereva kutoa bajaji zao wanapochoka, kuna muda hasa eneo la kupigia debe, dereva anaweza kumpa bajaji mtu mwengine aendeshe hata mpiga debe na hata huyo dereva yawezekana sio dereva rasmi wa hiyo bajaji kaazimwa tu kwa muda mchache hivyo anakimbizana na muda

Ni matumaini yangu kuwa hatua hizi zitasaidia kunyoosha tabia za madereva wetu bila kuwaharibia maisha yao kabisa, bali kuwajenga kuwa watumiaji wazuri wa barabara.
Wenu katika ujenzi wa taifa salama.
Leo siumeambiwa kulikuwa na mgomo wa daladala , wanagoma kushusha nauli
 
Ilikuwa purukushani nimepakua hio video mojawapo kwenye group, nimeona video nyingi maguta yamekuwa kama daladala
Ni shida sana isingekuwa konakona hapa malawi daladala zote ni kuzifutia leseni lakini pia walitakiwa Latra wawe na mwongozo wa nauli kulingana na bei za mafuta either ipande au ishuke sasa sielewi ofisini kazi yao ni nn
 
huyu kama ni kweli achukuliwe hatuw,
Tanzania bila ajari inawezekana
Shida imeanzia kwenye mgomo wa daladala, siku ya Leo Mbeya usafiri wa pikipiki (bajaji, maguta, boda) ulikuwa wa kugombaniwa sana.

Migomo hii imekuwa ikitokea mara kwa mara bila muafaka wa kudumu sababu ya conflicts if interests, baadhi ya mamlaka zinazohusika kutoa solution zina watumishi wanaomiliki bajaji na wengine wamezinunua kwa mkopo
 
Back
Top Bottom