Mbeya: CHADEMA wapinga agenda ya Katiba Mpya

Mbeya: CHADEMA wapinga agenda ya Katiba Mpya

Satoshi Nakamoto

Senior Member
Joined
May 28, 2017
Posts
110
Reaction score
464
Wanachama wa CHADEMA Mkoani Mbeya wamejitokeza kupinga agenda ya Katiba Mpya huku wakiwa wamevalia Tshirts za kuhamasisha Katiba Mpya!

IMG_20210731_203756_149.jpg

Source: TBC1 Habari
 
Unakataa kuvuta sigara huku moshi unatokea puani.

Aliyewashauri amewadharilisha sana,amewanunua mfanye uhuni bila mbinu sahihi. Aliyewanunua amejificha nyie mnabaki kutumika.

Asanteni kwa kuhamasisha umuhimu wa katiba mpya. CCM hoyeeee
 
View attachment 1875543
Wanachama wa CHADEMA Mkoani Mbeya wamejitokeza kupinga agenda ya Katiba Mpya huku wakiwa wamevalia Tshirts za kuhamasisha Katiba Mpya!

Source: TBC1 Habari
Waandishi wa TBC na Channel Ten wanajidharilisha sana kuto kubalance story. Maudhui ya mdomoni yanakinzana na mavazi yenye ujumbe unaohamasisha.

Waandishi muwe angalau mnawahoji baada ya matamko.Mnaiba kura halafu mnajiibia utashi wenu
 
Ndio maana vijana wakipewa uongozi wanaharibu.Uwezo wakuchambua mambo hawana.
Chalamila type!
 
Mhu! Huku kunaitwa 'kujipinga bila kujua kama unajipinga' (kutoa kauli 2 zinazopingana kwa wakati mmoja).
 
Aibu sana,ndio maana Rais amewateua DC wengi toka chadema wakati hawakutumika kuinua CCM.
Viongozi Taifa UVCCM wanagombana Diallo/Gwajima huku mdudu wanaishi naye

..kama kuna vijana wa chadema wanapinga katiba mpya hiyo ni haki yao ya kikatiba.

..haiwezekani ktk zama hizi kila mwanachama wa chadema akawa anaunga mkono katiba mpya.

..kinachonishangaza mimi ni kutokuona wanachama wa CCM wanaopenda katiba mpya kujitokeza na kueleza misimamo yao.

..pia nadhani siyo jambo la afya kwa CCM kufanya propaganda za kitoto-kitoto kujibu hoja ya katiba mpya.

..Nadhani kunajengeka UTAMADUNI wa CCM kutumia hila na propaganda kukabiliana na mawazo mbadala ktk jamii ya Watz. Hili jambo litaacha athari mbaya huko tunakokwenda.
 
Back
Top Bottom