Mbeya City Inaharibiwa na siasa za Simba SC na Yanga SC. Team ambayo ilipendwa sana na watu wengi

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
ilipoanza mbeya city ilianza kwa kishindo na kupata mashabiki wengi sana. iliiingia moja moja kuwa mshindi wa 3 katika ligi. huku ikiwa ni moja ya team zilizokuwa zikiogopwa sana. ilikuwa ina ushindani na wapenzi wengi waliipenda na kuifuatilia kwa ukaribu sana.

likaingia suala la simba na yanga. yanga wakawa wana watu wao wengi ndani ya mbeya city inasemekana kulianza kufanyika figisu figisu kuwa kila inapocheza na yanga iwe inapoteza kuisaidia yanga. hii hali imekuwepo kwa mud amfupi kutokana na kuwa na viongozi wengi ambao wana mapenzi na yanga ukianzia na aliyekuwa kocha mwambusi na viongozi kadhaa.

mechi ya juzi imekuwa na lawama sana hasa kwa baadhi ya wachezaji kuonekana kuwa wamecheza chini ya kiwango. inasemekana kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa sababu ya wachezaji kadhaa kucheza chini ya kiwango ili kuisaidia yanga. tabia hii imekuwepo sana katika hizi team kadhaa kubwa ambazo zimekwa zikifanya mchezo kama huu wa kununua wachezaji au kuharibu mpira.

watanzania,wapenda michezo mkoani mbeya msiache simba na yanga kuharibu team zenu ambazo zinakuwa na mahabiki wengi ambao ni mchanganyiko wa simba na yanga. tunafaham kabis asilimia 95 ya washabiki wa mpira nchini ni simba na yanga. baada ya hapo ndo huwa na mapenzi kwa team zao za mikoani. sasa mnapoanza tena kuziambatanisha na simba na yanga mnawakosea mashabiki wa mpira.
 
  1. Siasa serikali iliona timu inampaka kiki sugu
 
Ila Kweli mechi iliyopita ya Yanga vs Mbeya City ilikuwa ya uoande mmoja.
Wachezaji wa Mbeya City walicheza chini ya kiwango.
Inawezekana walichoka, au waliogopa Yanga au hawakuamka vizuri, mechi haikuwa na ushindani kama tunavyoijia Mbeya City.
Mbeya City ijihadhali yasije yakamkuta ya Toto Afrika.
 
Mbeya city toka imeanza ina unasaba na Yanga. Hali hii pamoja na nyingine itapelekea hii timu kushuka daraja siku za usoni. Viongozi wake kama kocha mwambusi na hata aliyekuwa afsa habari D 10 walikuwa mapenzi na Yanga na ndo maana wakaenda huko. Ijifunze kwa Toto na coastal ijiepushe na huu uñazi inawaviñja mashabiki Wake.
 
Vitimu vingine bana vikikutana na simba vina kamiaa kaa fainal.
 
Ila Kweli mechi iliyopita ya Yanga vs Mbeya City ilikuwa ya uoande mmoja.
Wachezaji wa Mbeya City walicheza chini ya kiwango.
Inawezekana walichoka, au waliogopa Yanga au hawakuamka vizuri, mechi haikuwa na ushindani kama tunavyoijia Mbeya City.
Mbeya City ijihadhali yasije yakamkuta ya Toto Afrika.
Msiwa wasakatonge na nyinyi!

Tafuta H2H ya Mbeya City na Yanga uone kuwa trend haibadiliki. Zimechezwa zaidi ya game 8 ambapo ni game 1 tu Mbeya City amemfunga Yanga.
 
demigod
mi nilikuwa natoa maoni tu, na sio msakatonge kama unavyodai.
Sio lazima umdhihaki mtu unayetofautiana naye kimawazo.
Punguza mhemko.
 
Malezi ndugu yangu kuna watu unaweza walaumu kumbe hawajapata malezi mazuri

demigod
mi nilikuwa natoa maoni tu, na sio msakatonge kama unavyodai.
Sio lazima umdhihaki mtu unayetofautiana naye kimawazo.
Punguza mhemko.
 
ilipoanza mbeya city ilianza kwa kishindo na kupata mashabiki wengi sana. iliiingia moja moja kuwa mshindi wa 3 katika ligi. huku ikiwa ni moja ya team zilizokuwa zikiogopwa sana. ilikuwa ina ushindani na wapenzi wengi waliipenda na kuifuatilia kwa ukaribu sana.

likaingia suala la simba na yanga. yanga wakawa wana watu wao wengi ndani ya mbeya city inasemekana kulianza kufanyika figisu figisu kuwa kila inapocheza na yanga iwe inapoteza kuisaidia yanga. hii hali imekuwepo kwa mud amfupi kutokana na kuwa na viongozi wengi ambao wana mapenzi na yanga ukianzia na aliyekuwa kocha mwambusi na viongozi kadhaa.

mechi ya juzi imekuwa na lawama sana hasa kwa baadhi ya wachezaji kuonekana kuwa wamecheza chini ya kiwango. inasemekana kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa sababu ya wachezaji kadhaa kucheza chini ya kiwango ili kuisaidia yanga. tabia hii imekuwepo sana katika hizi team kadhaa kubwa ambazo zimekwa zikifanya mchezo kama huu wa kununua wachezaji au kuharibu mpira.

watanzania,wapenda michezo mkoani mbeya msiache simba na yanga kuharibu team zenu ambazo zinakuwa na mahabiki wengi ambao ni mchanganyiko wa simba na yanga. tunafaham kabis asilimia 95 ya washabiki wa mpira nchini ni simba na yanga. baada ya hapo ndo huwa na mapenzi kwa team zao za mikoani. sasa mnapoanza tena kuziambatanisha na simba na yanga mnawakosea mashabiki wa mpira.
Mimi naitarajia na kuichukulia JF kuwa ni jukwaa la watu wenye fikra zilizokomaa ambao hawawachi utashi au dhana zao zikawa ndio chanzo cha mjadala. Kauli kama ‘inasemekana......’, ‘kulikuwa na jambo...’, zinapoambatana na tuhuma nzito za ‘tabia hii imekuwapo sana katika team hizi kadhaa kubwa’, ‘zimekuwa zikifanya mchezo kama huu wa kununua wachezaji au kuharibu timu’ zinamfanya myakinifu wa fikra kujiuliza kama mada ya aina hii ni stahiki kwa JF. Hoja hujengwa na hoja, haijengwi na dhana. Hoja ya kujengea hoja inapaswa kuungwa mkono na ushahidi kamili, mantiki ya kitaalamu na takwimu zinazokubalika kutoka vyanzo vinavyokubalika. ‘Inasemekana’, ‘kulikuwa na jambo’ si miongoni mwa mihimili hii ya kujengea hoja.
Wala mechi moja ya kufungwa mabao mengi haitoshi kuthibitisha kwamba kuna hujuma. La sivyo Scolari angeambiwa amekula njama na Ujerumani pale Brazil ilipofungwa 7-0 kwenye fainali ya Kombe la Dunia, kwa sababu tu ana asili ya Bara la Ulaya. Wala kocha kuwa na mapenzi na timu tofauti na anayoifundisha si kigezo cha kuihujumu timu hiyo. Timu ngapi za mataifa ya Afrika zimepata kufundishwa na makocha kutoka Ulaya, ambapo timu anayofundisha mwalimu huyo hukutana na timu ya Taifa la kocha huyo kwenye fainali za Kombe la Dunia?
Ni kweli Mbeya City kufungwa 4-0 inasikitisha. Lakini njia sahihi ya kujinasua ni kutafuta sababu, siyo visingizio.
 
demigod
mi nilikuwa natoa maoni tu, na sio msakatonge kama unavyodai.
Sio lazima umdhihaki mtu unayetofautiana naye kimawazo.
Punguza mhemko.

Msakatonge kwenye nadharia hii ya maa ni yule anaye lazimisha kukubalika kwa hoya yake issiyokuwa na mashiko..Sijakudhihaki hata hivyo!

sijawahi kuwa na mhemko utokanao na soka la bongo!
 
Mbeya city sijui wamerogwa nani kwa hii misimu miwili ya karibuni.

Mimi nilikuwa nawaita Atletico madrid ya bongo, walikuja kutoa challenge kubwa sana kwa vilabu vya simba na yanga.
 
Msiwa wasakatonge na nyinyi!

Tafuta H2H ya Mbeya City na Yanga uone kuwa trend haibadiliki. Zimechezwa zaidi ya game 8 ambapo ni game 1 tu Mbeya City amemfunga Yanga.
Mbeya city ilifungwa kwa mara ya kwanza na Yanga katika msimu wake wa kwanza wa vpl na ilkua on fire...
 
Tatizo simba wanataka washinde wao tu akishinda yanga kahonga, akifungwa ana njaa anashindia mihogo. Jamani hii ligi imekuwa ngumu kila mtu agangamale kivyake.
 
Wamempiga bao 7 JKT ruvu sisi tuka kaa kimya, Leo hii tunashinda bao 5 basi wapinzani wanaonkena kuwa wametuaachia. 😀
 
Mbeya city sijui wamerogwa nani kwa hii misimu miwili ya karibuni.

Mimi nilikuwa nawaita Atletico madrid ya bongo, walikuja kutoa challenge kubwa sana kwa vilabu vya simba na yanga.

Takwimu zinasema kwenye game 8 za mbeya na Yanga, Mbeya kashinda 1 tu. Unakaaje na kutegemea kuwa mtu kama huyu anaweza kuleta changamoto mbele ya Yanga..? Huyu huwa anamsumbua sana Simba, mara nyingi ushindi wa simba mbele ya Mbeya huwa na Margin ya bao 1 tu.

Mtibwa Sugar ndio tumuite Atletico Madrid.
 
Msakatonge kwenye nadharia hii ya maa ni yule anaye lazimisha kukubalika kwa hoya yake issiyokuwa na mashiko..Sijakudhihaki hata hivyo!

sijawahi kuwa na mhemko utokanao na soka la bongo!
Mimi sijamlazimisha mtu kukubaliana na hoja yangu popote.

MSAKATONGE maana yake ni mtu mwenye njaa na anayefanya chochote hata kisichokubalika na Jamii ili apate kutimiza mahitaji yake ikiwemo na hitaji la kupata chakula.

Unahitaji kuwa na busara na pia kuelewa maana ya maneno unayoyatumia.
 
Back
Top Bottom