Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 252
Klabu ya Mbeya City Fc, tumesikitishwa na habari iliyotolewa na gazeti la Mwanaspoti toleo Namba 1731 la tarehe 17-18 March 2015 yenye kichwa cha habari
Mbeya City yatimua kocha
Hii ni habari ya uwongo na uzushi mkubwa ambayo mwandishi ameandika kwa utashi wake bila hata nukuu yoyote kutoka uongozi wa Mcc fc.
Ndani ya timu jana jumatatu hakukuwa na kikao chochote cha viongozi wala aina yoyote ya mazungumzo kuhusu Kocha Juma Mwambusi.
Tunaomba ieleweke kuwa Juma Mwabusi ni kocha wa Mcc fc na hakuna habari nyingine yoyote nje na hiyo.
Wito wetu kwa wana habari ni vizuri kupata taarifa rasmi kutoka mamlaka husika badala ya 'kukurupuka' na kuandika habari za uongo ambazo kwa namna moja ama nyingine huchafua taswira ya tasnia hii muhimu.
Chanzo: Mbeya City Official