Mbeya City yakanusha kufukuza kocha

Mbeya City yakanusha kufukuza kocha

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
252
Klabu ya Mbeya City Fc, tumesikitishwa na habari iliyotolewa na gazeti la Mwanaspoti toleo Namba 1731 la tarehe 17-18 March 2015 yenye kichwa cha habari
Mbeya City yatimua kocha
Hii ni habari ya uwongo na uzushi mkubwa ambayo mwandishi ameandika kwa utashi wake bila hata nukuu yoyote kutoka uongozi wa Mcc fc.
Ndani ya timu jana jumatatu hakukuwa na kikao chochote cha viongozi wala aina yoyote ya mazungumzo kuhusu Kocha Juma Mwambusi.
Tunaomba ieleweke kuwa Juma Mwabusi ni kocha wa Mcc fc na hakuna habari nyingine yoyote nje na hiyo.
Wito wetu kwa wana habari ni vizuri kupata taarifa rasmi kutoka mamlaka husika badala ya 'kukurupuka' na kuandika habari za uongo ambazo kwa namna moja ama nyingine huchafua taswira ya tasnia hii muhimu.

11054422_878366315538621_213722167667380094_o.jpg



Chanzo: Mbeya City Official
 
Mbeya City kwanini wanamng'ang'ania sana Huyu kocha wakati timu inaboronga kila siku? au ni masharti ya mganga wao?
 
mwanaspot siku hizi limekuwa kama gazeti la udaku ukisoma vichwa vya habari haviendani na habari yenyewe
 
kiukweli kwa sasa sijui tusome gazeti gan la michezo kwenye mitandao maana mwanaspoti kiukweli limepoteza credibility kabisa. limekuwa gazeti la udaku sana na habari zake hata zinavyoandikwa zinaandikwa kiudaku udaku. kichwa cha hbr na hadithi yenyewe mara nyingi vinakuwa havifanani ni sawa na kichwa cha habar cha gazeti la udaku kinachoandikwa "Rais afumaniwa " unakuja kusoma unakuta ni Rais wa masharobaro
 
Back
Top Bottom