Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Rekodi ya sare yaendelezwa katika dimba la Sokoine kati ya Mbeya city dhidi ya Yanga baada ya mchezo uliochezwa hii leo kumaliza kwa matokeo ya 1-1.
Goli la Yanga limefungwa na D Kaseke dakika ya 84 . Huku goli la Mbeya city likifungwa na P Athanas kwa mkwaju wa penati kunako dakika ya 90 +4.
Kwa matokeo haya Yanga anaendelea kusalia katika nafasi ya kwanza akiwa na alama 45, huku Mbeya city akipanda nafasi moja juu kutoka ya 18 hadi 17 akiwa na alama 15.
Katika mchezo wa awali Mwadui fc alikuwa nyumbani kuikaribisha Biashara United mchezo ambao umeishuhudia Biashara United ikiibuka kidedea baada ya magoli yaliyofungwa dakika za lala salama kuiandikia ushindi wa bao 2-1.
Goli la Mwadui lilikuwa ni goli la kujifunga lililowekwa kimyani na A Mangalo dakika ya 85 , na magoli ya Biashara yakifungwa na Y Athman dakika ya 90+1 na G Kabeja dakika ya 90 +4.
Kwa matokeo hayo Mwadui fc anashuka nafasi moja chini na kushika mkia katika msimamo wa ligi huku Biashara akiendelea kujichimbia katika nafasi ya 4.