PreGE2025 Mbeya: Dkt. Tulia Ackson afuturisha Waumini 200 wa dini ya Kiislam

PreGE2025 Mbeya: Dkt. Tulia Ackson afuturisha Waumini 200 wa dini ya Kiislam

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambaye ni Spika wa Bunge, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) na Mbunge Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson imetoa futari kwa waumini 200 wa dini wa kiislam.

Futari hiyo imekabidhiwa leo Jumatano, Machi 19,2025 kwa Shekhe Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha na Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust Jackline Boaz.

1742540336755.png

​
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika makabidhiano hayo Njalambaha amesema watanzania wanapaswa kuliombea taifa kuelekea uchaguzi Mkuu ili uwe wa amani na utulivu kwa maslai ya Taifa na watanzania.

"Tuna tunu za kujivunia kama Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge Dkt,Tulia Ackson tunawaomba tutunze hizo tunu za taifa letu," amesema.

Naye Mjumbe wa Baraza la Mashekhe Mkoa wa Mbeya, Ibrahim Bombo pamoja na waumini walipewa Futari hiyo wameishukuru Taasisi hiyo chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Tulia kwa namna anavyoigusa Jamii yenye mahitaji.

 
Hajui kwamba kuna kwaresma na ndio waumini wengi wapo huko? Amekariri vibaya sana tunasubiri alete comwe mwezi wa 10
 
Back
Top Bottom