Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Mitaa ya Mbeya kuna “njemba” zimepewa tenda za kukusanya taka kwenye kila kata lakini zinaweza kupita siku tatu hadi nne gari ya taka haijapita kubeba taka sasa sijui pesa za taka wanakusanya kwa ajili ya nini.
Sasa tuachane na huo uchafu ambao wenye mamlaka wameonekana kushindwa kutatua tatizo hilo.
Nahamia kwenu ninyi ndugu zangu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Jijini Mbeya, hivi kuhusu hizi chemba zinazovujisha maji mitaani ni kwamba hamna taarifa nazo au ndiyo mnatukomoa?
Tunajua lengo lenu la kuanzisha mradi huu wa maji taka lilikuwa zuri tu la kutufanya tuachane na vyoo vya shimo lakini mbona sasa hivi limegeuka kuwa kero kubwa sana kwetu Wananchi?
Mtandao wa majitaka ni mfumo wa kutandika mabomba katika sehemu mbalimbali za makazi ya watu kwa ajili ya kukusanya maji yaliyotumika na kuyasafirisha kwenda maeneo yaliyotengwa.
Kwasasa imekuwa tofauti maji taka hayo badala ya kuyakusanya na kuyapeleka kwenye Malambo yaliyopo eneo la Kalobe sasa yanatapakaa mitaani.
Mabomba ya Majitaka yenye urefu wa km 105 yametandikwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji hili kama vile Forest ya zamani, Jacaranda, Itiji, Iyunga sehemu ya viwandani, Sisimba, Mwanjelwa, Ikuti, Uhindini, Sokomatola, Majengo, Mbalizi road, Forest mpya, Block T, Ruanda, Simike, Kalobe, Ilolo, Isanga na Uzunguni.
Sasa katika baadhi ya maeneo hayo, kwa mfano Forest ya Zamani eneo la Shule ya Sekondari ya Sangu karibu na Bustani ya maua kuna chemba inavujisha maji ambayo yanaingia kwenye mtaro unaoelekea Ilolo ambako ni maarufu kwa kilimo cha Mboga mboga.
Ukiachana na Chemba hiyo kuna nyingine iko maeneo ya Mtaa wa Meta Sekondari hii nayo ina balaa lake, inatiririsha maji taka kwa Saa 24.
Ukipita Ilolo huko ndiyo usiseme maana maji taka yamekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wakazi wa maeneo hayo.
Mbaya zaidi Kuna hii ya pale nyuma ya Shule za River Side na Mbeya Sekondari yaani inatiririsha maji taka mpaka imetengeneza kibwawa ambacho kimekuwa kinaleta kero Kwa wanafunzi na wapita njia wa eneo hilo katika Kata ya Simba.
Kuna maeneo mengine mengi tu ambayo yamekuwa na changamoto hizi za chemba kutiririsha maji taka.
Wananchi mliyotufungia huu mradi tuna lipia Ankara, hivyo tunapowapigia simu mafundi wenu kuwapa taarifa za changamoto hizi wanatakiwa Kuja kuzibua na siyo kuanza kutudai malipo.
Maana mafundi wenu wamekuwa wakidai malipo kutoka Kwetu ili wazibue hizo chemba na kwa vile tunaopata shida ni sisi tuna lazimika kulipa.
Ninyi viongozi wa mitaa hivi hizi changamoto hamzioni kweli au mnatufanyia makusudi maana mtu unamfuata kiongozi wa mtaa kumuelezea changamoto anakwambia nitafuatilia lakini kila kukicha hali ni ileile, Mwanongwa nawakumbusha viongozi kuwa sisi wananchi wenu ndiyo maboss zenu hivyo mnatakiwa kututumikia kwa nguvu zenu zote.
Sasa ndugu zangu wa mamlaka ya maji safi na maji taka Jiji la Mbeya nawakumbusha kuwa tunaelekea kipindi Cha masika,chonde chonde zile chemba ambazo zimekuwa sugu au niseme zile chemba ambazo hamtaki kuzizibua basi jitahidi jamani mzifanyie kazi maana msimu wa masika umefika na kipindi hiki ndiyo kunakuwa na magonjwa mengi ya mlipuko hivyo ni vyema mkaweka miundombinu yenu vizuri.
Mwisho kabisa siwezi kuwaacha salama ninyi Binadamu wenye tabia ya kuiba mifuniko ya chemba,embu acheni hiyo tabia maana pia ni chanzo Cha kuzifanya hizi chemba kuvunisha maji pindi zinapoziba.
Najua tunaelekea Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nawaomba wananchi wenzangu tujitokeze Kwa wingi kupiga kura ili tuweze kuwapata viongozi ambao watatusikiliza na kutatua shida zetu,kama kiongozi unajijua ulishindwa kuwasaidia wananchi wako nakushauri usichukue fomu.
Ni hayo tu niliyokuwa nayo ndugu yenu Mwanongwa