Mbeya: Kijana wa Miaka 17 ahukumiwa kifungo cha nje Miezi miwili kwa kumbaka Mwanafunzi

Mkuu hatutumii hisia kufanya maamuzi, ni sheria ndo zilivyo. Mtoto wa miaka 17 ni "criminally liable". Yaani unataka kusema vitoto vya miaka 15-17 vifanye makosa ya jinai halafu viachwe tu!!!
Kwahiyo huyo binti wa miaka 17 yeye hastahili kuadhibiwa!?
Kumbuka hao wamekutana kwa makubaliano hadi kujamiiana japo mwanaume ndio kaonekana kamlaghai mwanamke.
Kisayansi mtoto wa kike ana rapid mind growth and development kuliko mwanaume hadi afikiapo miaka 16.
Inamaana tukitizama bint alikua na uwiano sawa wa kifikra na kimaamuzi sawa na kijana.
Kuna muda sheria huwa zinachekesha sana.
 
Hizi kesi Zipo africa tu lakini uku kwa wazungu hakuna kesi kama hiyo
Dada Yangu uku mwaka 2022 alikuwa bado ana umri wa miaka 15 alianza mausiano na jama mmoja mwenye umri wa miaka 26 jana alimpa ujauzito akamlazimisha otowe kwasababu alikuwa bado mtoto , Dada akaanza kuumwa kidogo kufa alikuwa hapa na hapa hospital
Siku moja rafiki yake ya Yule kijana ndo akatuambia ukweli kuhusu kilichotokea
Familia tukajua
Tukaenda kushtaki kijana Yule kasi akaanza kijana hakushikwa wala nini alipewa kifungo cha nje
Kufika mwaka huu ikapelekwa kwa hakimu ili atoe hukumu
Hukumu ambayo ilitolewa mpaka Sasa najiulizaga huu uchawi au ni sheria za canada
Baada ya Dada yangu kutowa malalamiko yake hakimu akatowa hukumu kwa kufuta kesi eti walikuwa wanapendana hakuna kesi
Mpaka Sasa najiulizaga maswali mengi sipatagi majibu
Mapenzi ya 15 na 26
Mda mwingine nafikiriaga labda ni ubaguzi au nini
Kwa ufupi wazugu hawanaga mambo ya sauti ya mtoto isikike
 
Kubaka na kutia mimba faini laki 2 na kifungo cha nje miezi 12, tusubiri mimba zingine za kutosha km mwendo ndio huo miezi 12 nje kitu gani laki 2 kitu gani zitapigwa mimba huko mpaka mahakimu wakose pa kuziweka kesi
 
Hiii haiwezi kuwa Canada ninayoifahamu Mimi na hizo harsh gynocentric laws walizonazo.
 
Sheria Ile Ile Kwa kosa lile lile katika nchi Ile Ile yenye kanuni Ile Ile ya adhabu Kwa makosa ya jinai Ile Ile lakini uzito wa adhabu Kwa washukiwa ni tofauti tofauti.
Daah mnaosoma Sheria endeleeni kusoma mi siiwezi maana vinginevyo ningekuwa Mungu Mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…