Mbeya: Kijana wa miaka 27 atupwa Jela miaka 30 kwa kumbaka Mwanafunzi wa miaka 12

Mbeya: Kijana wa miaka 27 atupwa Jela miaka 30 kwa kumbaka Mwanafunzi wa miaka 12

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jebras Jaluwa [27] Mkazi wa Kijiji cha Ikukwa Wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mshewe.

Hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 63/2022 imetolewa Aprili 19, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mbeya Mjini baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 11, 2022 huko Kijiji na Kata ya Mshewe, Wilaya ya Mbeya vijijini baada ya kumlaghai mtoto huyo kwa kinyume na kifungo namba 130 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shitaka lake, alikiri kutenda kosa ndipo Hakimu alitoa hukumu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia na tamaa za kimwili kama yake.
 
Mbeya na Malawi ni pua na mdomo alikwama wapi huyo mpuuzi?
 
Back
Top Bottom