Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Wadau niko mbeya kwa ajili ya maonesho ya nane nane, nimeona mwitikio ni mkubwa sana ,unaweza kupotea ulikotokea ,hii imenipa picha kwamba watanzania wana kiu ya kusikia kero za kilimo zinatatuliwa.
Nchi yetu kwa sasa haina chakula kabisa. Hata hawa NMC hawana akiba tena. Tutasingizia mvua ilikuwa haitoshi lakini hapana mimi nachojua wakulima walishindwa kumudu bei ya pembejeo. Kama yale maeneo yanayozalisha chakula tungeyapa kipaumbele mahindi yangekuwa mengi sana
Serikali angalieni maeneo kama Rukwa, Mbeya, Ruvuma na Katavi ikiwezekana wakopesheni hawa wakulima pembejeo kama mbolea na mbegu mtakuja kunishukuru.
Benki ya kilimo mikopo yake ni migumu kwa wakulima wa vijijini kuipata na masharti yake ni magumu , pelekeni mbolea Rukwa na maeneo mengine ya kimkakati. Wakopesheni mbolea mkifanya hivyo hata vijana wanaokaa vijiweni watalima