BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mbeya yaendelea kuwa gizani
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Tuesday,November 25, 2008 @21:15
Mkoa wa Mbeya jana uliendelea kuwa katika giza totoro kwa siku ya tatu mfululizo, baada ya transfoma linalopokea umeme kutoka katika Gridi ya Taifa na kuusambaza mkoani hapa, kupata hitilafu Jumapili iliyopita.
Kutokana na hitilafu hiyo ya umeme, shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Mbeya vikiwamo viwanda vidogo, mafundi mchundo, vinyozi, sehemu za mitandao zimekwama kuendelea na shughuli za kila siku na kusababisha wananchi wanaotegemea shughuli hizo kuwa katika hali ngumu kiuchumi.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mbeya, Mhandisi Stella Hiza alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, mafundi sita kutoka Dar es Salaam wamewasili hapa kuungana na mafundi wengine ili kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo, alisema hawezi kusema ni lini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi na kwamba wanajitahidi usiku na mchana katika kuhakikisha transfoma hiyo inatengenezwa na kuendelea kupokea umeme kutoka Gridi ya Taifa na kuwawezesha wananchi kuendelea kupata huduma kama kawaida. Baadhi ya wananchi walisema kukatika huko kwa umeme kusikokuwa na kikomo kumesababisha kukwama kwa shughuli za kiuchumi, na Tanesco wanatakiwa kuhahakikisha wanarejesha haraka huduma ya umeme.
Katika taarifa yake juzi, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema transfoma kubwa inayosambaza umeme kwa mkoa huo iliyopo katika kituo cha umeme cha Mwakibete, imeharibika ghafla Jumapili iliyopita. Alisema jitihada za kutengeneza transfoma hiyo zinafanywa kati ya Tanesco Makao Makuu na Mbeya, na kuwaomba radhi wananchi wote wa Mbeya kutokana na usumbufu unaojitokeza kutokana na tatizo hilo.