Mbeya: Magari yanateketea kwa moto kijiji cha mwale Chimala

Mbeya: Magari yanateketea kwa moto kijiji cha mwale Chimala

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Moto mkubwa unawaka muda huu kijiji cha mwale Chimala mkoani Mbeya malori ya mafuta yanateketea na moto chanzo cha ajali bado hakijulikani. Malori ya mafuta yanawaka moto ni balaa

Ni pale hapo stendi mpya karibu na dukani kwa Mama Pipo.

=====

MOTO WATEKETEZA MAGARI 6 NA NYUMBA 4 MBEYA

Taarifa iliyothibitishwa na Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ayoub Sanga, imeelezwa kuwa Magari 6, Pikipiki 2 na Nyumba 4 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huko Chimala Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya

Diwani wa Kata hiyo, Charles Komba amesema moto huo ulianza majira ya saa nne usiku kutoka kwenye Lori lililokuwa limeegeshwa katika kituo maalumu cha magari maarufu kama Mama People

Zimamoto lilifika saa 6 usiku na kufanikiwa kuzima moto huyo ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni biashara holela ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokuwa ikifanywa na madereva katika eneo hilo.

#JamiiForums #JFMatukio
 
Naona ni mtindo mpya sasa,wiki tatu zimepita gari ya mafuta ilichomwa inyala wanakijiji waliacha vitanda wakalala mtoni
 
Moto mkubwa unawaka muda huu kijiji cha mwale Chimala mkoani Mbeya malori ya mafuta yanateketea na moto chanzo cha ajali bado hakijulikani. Malori ya mafuta yanawaka moto ni balaa

Ni pale hapo stendi mpya karibu na dukani kwa Mama Pipo.
View attachment 2330852
Umechukua video kwa mbali sana. Ungesogea karibu tungepata kuona hadi chanzo cha moto
 
Hapo hamna hata moja lenye mafuta. Tumerudia mambo yetu yale.
 
Hiyo itakuwa kwamba alikuwa anaiba temperature akajisahau akawasha fegi.

Dhana tu.
 
Huwa wanapak sehemu Ili kupakua mafuta nadhan
Ilitokea pale Nyakanazi watu walikuwa kazini moto ukawaka Gari za Petroli na Diesel na watu wakaangamia.

Nchi hii ina Matrafiki wa ajabu sana unakuta kazipiga mkono Gari za Mafuta na za Amonium Nitrate sehemu moja kwa sababu ya buku buku zake,sasa hebu fikiria kukitokea moto?!.
 
Moto mkubwa unawaka muda huu kijiji cha mwale Chimala mkoani Mbeya malori ya mafuta yanateketea na moto chanzo cha ajali bado hakijulikani. Malori ya mafuta yanawaka moto ni balaa

Ni pale hapo stendi mpya karibu na dukani kwa Mama Pipo.
View attachment 2330852
Hiyi barabara aliyokataa kuitengeneza mwendazake sasa inakula vichwa na kuleta balaa!
 
Back
Top Bottom