Mbeya: Magari yanateketea kwa moto kijiji cha mwale Chimala

Mbeya: Magari yanateketea kwa moto kijiji cha mwale Chimala

Alaumiwe kinana kwa kutoa maaskari barabarani
 
Alaumiwe kinana kwa kutoa maaskari barabarani
 
Alaumiwe kinana kwa kutoa maaskari barabarani, madereva wa TANZANIA ni SAwa na mbuzi wasipochungwa lazima ajali ziwe nyingi
 
Na sio lazima kupaki barabarani mbona nje ya barabara yapo maeneo
Mara nyingi unakuta pamejaa sasa kama umechoka na una usingizi unatafuta sehemu ambayo unahakikisha uko nje ya lami.
 
Moto mkubwa unawaka muda huu kijiji cha mwale Chimala mkoani Mbeya malori ya mafuta yanateketea na moto chanzo cha ajali bado hakijulikani. Malori ya mafuta yanawaka moto ni balaa

Ni pale hapo stendi mpya karibu na dukani kwa Mama Pipo.
View attachment 2330852
Taarifa iliyothibitishwa na Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ayoub Sanga, imeelezwa kuwa Magari 6, Pikipiki 2 na Nyumba 4 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huko Chimala Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Diwani wa Kata hiyo, Charles Komba amesema moto huo ulianza majira ya saa nne usiku kutoka kwenye Lori lililokuwa limeegeshwa katika kituo maalumu cha magari maarufu kama Mama People.

Zimamoto lilifika saa 6 usiku na kufanikiwa kuzima moto huyo ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni biashara holela ya mafuta ya petroli na dizeli iliyokuwa ikifanywa na madereva katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom