The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya-UWSA), CPA Gilbert Kayange, amefanya ziara ya mtaa kwa mtaa katika Jiji la Mbeya kwa lengo la kukagua miundombinu ya maji, kusikiliza kero za wananchi, na kutatua changamoto mbalimbali za kihuduma kwa wateja wa mamlaka hiyo.
Katika ziara hiyo, akiongozana na watumishi wa Mbeya-UWSA, CPA Kayange amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi, ikiwemo wizi wa mita za maji na uharibifu wa miundombinu unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu ili kujipatia huduma ya maji kinyume cha sheria.
CPA Kayange ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu wizi wa maji na mita za maji. Ametangaza zawadi ya Shilingi milioni moja (1,000,000/=) kwa yeyote atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa kwa wahalifu wanaohujumu miundombinu ya maji.
"Uharibifu wa miundombinu husababisha hasara kwa serikali, upotevu wa mapato, na kuathiri upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa wananchi," amesisitiza CPA Kayange.
Kwa hatua hii, Mbeya-UWSA inaendelea kuimarisha juhudi za kuboresha huduma za maji safi na kuhakikisha kuwa miundombinu ya maji inalindwa ili huduma hiyo muhimu iwe endelevu kwa wakazi wa Mbeya.
Chanzo: Jambo TV