Mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Mtoni, Kata ya Ruanda, jijini Mbeya kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Elisha Chonya, ameyakataa matokeo akidai kanuni zilivunjwa huku msimamizi wa uchaguzi Bi. Winifrida Stanley akitangaza matokeo ambapo Bilali Gembe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kura 95 dhidi ya wapinzani wake, Elisha Chonya (CHADEMA) aliyepata kura 68 na Issa Gawaza (CUF), aliyepata kura mbili.
Licha ya kutangazwa matokeo hayo, Bw. Chonya amesema kwa sababu ya mambo mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa zoezi la kupiga kura, anakwenda kufungua kesi Mahakama ya Wilaya.
Wapinzani kuendelea kulalamikia Rafi za Uchaguzi wakati tatizo la msingi lipo wazi na linaeleweka ni kupoteza muda kabisa.
Yeye ndo aliyeandaa na kusimamia uchaguzi, Mahakama ipo mikononi mwake, Bunge lipo mikononi mwake, vyombo vya ulinzi na usalama vipo mikononi mwake, hapo kuna nini zaidi ya shida tupu?