Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Naona miradi inaendelea kukamilika kwa kasi ya ajabu kabla ya Uchaguzi Mkuu.
CCM theatrics zenu tunazijua
==========================================
Mradi wa maji Luduga-Mawindi wilayani Mbarali Mkoani Mbeya awamu ya nne umetekelezwa kwa kutumia Mkandarasi GNMS CONSTRUCTIONS LTD ambapo ulianza kutekelezwa mnamo 28/03/2022 na kukamilika 28/02/2025 na gharama ya Mradi ni Tsh. 5,232,737,680.93 na chanzo cha fedha cha mradi huu ni Mfukuko wa Maji wa Taifa (NWF).
Mradi huu ni mwendelezo wa awamu tatu zilizopita zilizopelekelea kufikisha maji kwenye kijiji kimoja cha Kangaga, ambapo awamu hii ya nne imeweza kufikisha maji katika vijiji vitano vya Manienga, Itipingi, Mkandami, Matemela, pamoja na Ipwani, na chanzo cha mradi huu ni Mto Mpeng’o unaopatikana katika Kijiji cha Luduga Wilaya ya Wanging’ombe katika Mkoa wa Njombe wenye uwezo wa kuzalisha maji mita za ujazo 84,672 kwa siku.
Mradi huu unahusisha ujenzi wa mtandao wa bomba kilometa 91.62, ujenzi wa matanki matano yenye uwezo wa kuhifadhi maji jumla ya Lita 475,000, Ujenzi wa vituo 44 vya kuchotea maji na ujenzi wa ofisi ya chombo cha kutoa huduma ya maji (CBWSO).