Mbeya: Mwalimu anayetuhumiwa kumshushia kipigo Mwanafunzi aliyedokoa maandazi ashikiliwa na Polisi

Mbeya: Mwalimu anayetuhumiwa kumshushia kipigo Mwanafunzi aliyedokoa maandazi ashikiliwa na Polisi

Huyo mtoto lazima kuna kosa alitenda ndiyo maana akapewa adhabu ya kulala njaa.

Ilibidi lihojiwe kwanza kosa gani alitenda hadi kupelekea kulazwa njaa kisha kama lina mantiki ahojiwe huyo mtoto kwanini asiitumikie adhabu yake ya kwanza akaenda kutenda kosa lingine la wizi?inaanza hivi hivi kesho ametetewa anamaliza form six anaingia chuo anaendeleza tabia za wizi kwa vitu vya wanachuo wenzake kesho anamaliza anapata ajira yeye atawaza kuiba tu balaa akikosa ajira akarudi mtaani anakuwa mkabaji.

Wengine sisi illibidi tuwe wezi ila tupo tulivyo sasa kwa sababu ya ushirikiano wa walimu na wazazi wetu,mwalimu asishushwe thamani akienda wrong aitwe kisiri aonywe hizi tabia za matamko kuwakaripia walimu kama watoto wadogo zinawapa hao watoto fursa ya kuwadharau na kuwaona kumbe hawawafikii hata baba zao kwa sababu hawajawahi kuwaona wakikaripiwa yet hawajui baba zao hawawezi kuwapa wanachopewa na waalimu wao.
 
Viboko muhimu sana madogo hawaelewi ,hawasikiii

Namuunga mkono Ticha
 
Kumnyima tu mtoto chakula ni kosa tena lisilo la kibinadamu. Mkuu wa shule Naye ahojiwe.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Ukisikia polisi wanasema taarifa inaandaliwa ujue kweli inaandaliwa.
 
Kumnyima tu mtoto chakula ni kosa tena lisilo la kibinadamu. Mkuu wa shule Naye ahojiwe.
Kuna ushahidi gani amenyimwa chakula?

Huyu ni mkora wa mandazi ila kama kapewa kipigo heavy sio sawa apewe kichapo cha wastani maisha yaendelee.
 
Kufuatia kuripotiwa kwa tukio la Laurence Nicholaus Mwangake, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Rohila, Mbalizi kulazwa Hospitali ya Ifisi tangu Februari 12, 2023 ikidaiwa amejeruhiwa kwa kipigo, watuhumiwa wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju anaelezea klichotokea:
"Taarifa zinaeleza Mwanafunzi alidokoa maandazi manne, walinzi wakamuona, wakamkamata na kumzuia kwenye chumba cha darasa wakiwa na Mwalimu aliyefahamika kwa jina la Petro Kamili, ambapo wakamdhibiti kwa kumfungia katika chumba hicho.

"Inaelezwa kuwa kitendo cha kudhibitiwa katika chumba huku Mwanafunzi akiwa na rekodi ya kuogopa kuchapwa, akaruka kwa nia ya kutoka kwenye darasa hilo kupitia dirishani, kitendo kilichosababisha apate majeraha kadhaa kwa kuwa kuna kioo ambacho kilimjeruhi.

"Baada ya tukio hilo kujulikana kwa Mkuu wa Shule, akaamua kumhoji mwanafunzi ambaye amedai kuwa alinyimwa chakula, hivyo wakati wa kulala akashindwa kuvumilia akaenda kudokoa maandazi hayo maandazi manne kwenye duka la Shule.

“Mkuu wa Shule akawasiliana na Polisi kwa hatua zinazofuata za kiusalama.
"Pia niweke sawa maelezo tuliyopata yanaeleza kuwa siyo Walimu wanne na walinzi wawili waliomshambulia mwanafunzi kama inavyosemwa, bali mhusika ni Mwalimu mmoja na mlinzi mmoja ambao hivi ninavyozungumza wanashikiliwa na Polisi tangu jana (Februari 14, 2023) kwa mahojiano.

“Sisi pia tunaendelea kufuatilia kwa kuwa Mwalimu anadai yeye hakumchapa bali Mwanafunzi alijirusha mwenyewe dirishani, hivyo muhimu kwa sasa ni kuangalia afya ya Mwanafunzi wakati uchunguzi unaendelea kwa kuwa Mwanafunzi anasema yake na Mwalimu anasema yake pia.”

RPC ANENA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga amesema: "Taarifa inaandaliwa kuhusu tukio hilo, ni kweli hilo suala lipo na wahusika wawili tunawashikilia ambao ni Mwalimu na Mlinzi, nitatoa taarifa kamili muda si mrefu."

Pia Soma: Mbeya: Mwanafunzi alazwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Rohila, inadaiwa alidokoa maandazi manne
Mbona dakitari aliyemtibu alisema mwanafunzi mwenyewe alimuambia aliumia baada ya kuruka dirishani.
 
Hivi hawa walimu wanaishi nchi gani kiasi cha kutokujua yanayowahusu kuhusu kuhusu kuadhibu wanafunzi? Ya nini kuadhibu mwanafunzi wakati jamii inaona wanafunzi wanafanyiwa ukatili? Ni kuwaacha tu wanafunzi wajifanyie wanavyotaka ili jamii ivune inachopanda. By the way mimi kama mwalimu sitaacha kutoa adhabu kali kwa mwanafunzi yeyote atakayeonesha utovu wa nidhamu hata kama jamii nzima iko kinyume na mimi. Sitakubali maadili yamomonyoke, sikulelewa hivyo wakati nasoma niliadhibiwa nilipokwenda kinyume na walimu wangu walionifundisha na haukuwa ukatili. Hizi ni kampeni za kipuuzi na hazikubaliwi kabisa kuacha kuwatembezea viboko wanafunzi. Cha msingi ziwe ni adhabu za kawaida na nyepesi zisizojeruhi na kuua. Adhabu za kufukua visiki, kulima nyasi, kufanya usafi maeneo ya shule bila kuacha kucharaza viboko ikibidi iwe hivyo.
 
Ndiyo maana nasema walimu wengi ni vilaza. Huna Akili wewe kuku
 
Polisi Polisi Polisi! Hivi lini mtaacha uongo?? Taarifa zimeshatangazwa na bwana Kuzaga ukasema huna taarifa hujafuatilia kwa sababu una wageni, leo unasema kupitia wasiri wako wasiri gani na siri gani hapo??!

Mama Samiah Suluh Hassan alishasaini sheria ya kukataza kumuweka mtuhumiwa ndani kabla ya kukamilisha uchunguzi je nyie mko juu ya sheria hiyo au kwa sababu mahabusu kwenu ni chanzo cha mapato haramu ndio maana hamtaki kutii sheria hiyo?! Jirekebisheni mnatia kichefuchefu.
 
Na huyo mwanafunzi mwizi kachukuliwa hatua gani? Au wanamlea aendelee kuwa mwizi ili aje kuchomwa moto au auwawe na polisi kwa kusema richamaa ririkuwa richambasi ssugu?!
 
Ndiyo maana nasema walimu wengi ni vilaza. Huna Akili wewe kuku
walimu watadharaulika sana kama asipotokea wa kuwatetea, wao wenyewe hawajitetei japo wana chama chao. Chama chao kinatetea mambo ya hela tu lakini heshima ya walimu ikitwezwa hakitetei. Mimi kama mwalimu daima nitatetea heshima ya walimu ikibidi kuwa hivyo. Mwalimu ndiye kila kitu katika dunia hii
 
You can't get A performance by using C performers. Walimu hawawezi kutusaidia.
 
Most of the teachers in our country are suffering from psychological problems someone need to realize it and give them immediate help and attention.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Wakati ni hukumu nzuri sana walimu wanatuhumiwa ila hawana mtetezi wakati utakua mtetezi wao mzuri maa a maadili yanazidi kuteketea jamii hii ngoja tuone . Time Will tell
 
Back
Top Bottom