Mbeya: Mwamba auza sehemu ya pori la akiba Rungwa

Dah
 
Kuna mtu alishataka kuniuzia sehemu ya pori la akiba ekari moja akawa anauza 100,000 tzs nilikuwa mbioni kununua kama siyo yeye kujichanganya.
 
Mtu utanunuaje eneo kubwa kama hilo bla kuonyeshwa na kwenda kuhakiki documents za umiliki, upimaji na vielelezo vingine?? anayetakiwa kuwajibika ni huyo mnunuzi na akili zake nusu....Mjinga kabisa
 
Huyo serikali kaifanya kama yake kuuza hifadhi.nakwnn mwenyekiti wa kijiji cha mkola hapo kitunda aliuza na hakushikwa kwnn huyo atafutwe na mwenyekiti huyo wamsake ashikwe alikula hela nyingi mno za wafugaj
 
#HABARI Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani humo kumsaka na kumtia nguvuni, Andrea Ngomeni, mkazi wa Kijiji cha Kambikatoto wilayani Chunya kwa tuhuma za kuuza eneo la pori la akiba la hifadhi ya msitu wa asili Rungwa.

Homera ametoa agizo hilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya baada ya kufika katika hifadhi na pori la Rungwa Two na kukuta sehemu ya hifadhi imefyekwa kwa ajili ya kilimo na mifugo na kujulishwa kuwa eneo hilo limeuzwa kwa wafugaji kutoka wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

"Nawaagiza polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kumsaka huyu bwana Andrea akamatwe ili hatua zichukuliwe, maana haiwezekani watu wanajifanyia wanavyotaka," amesema RC Homera

#EastAfricaTV
 
Hii habari,ilishaletwa humu na huyo mwamba aliyejimegea keki ya taifa
Alishadakwa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…