DOKEZO Mbeya: Mwanafunzi alazwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Rohila, inadaiwa alidokoa maandazi manne

DOKEZO Mbeya: Mwanafunzi alazwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Rohila, inadaiwa alidokoa maandazi manne

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kijana Laurence Nicholaus Mwangake mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Rohila iliyopo Mbalizi Mkoani Mbeya amelazwa Hospitali ya Ifisi ikidaiwa amejeruhiwa vibaya na Walimu wanne pamoja na Walinzi wawili wa shuleni hapo.

1676463192072.png
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shule ya Rohila zinaelezwa kuwa chanzo ni baada ya Mwalimu kumtuhumu mwanafunzi huyo kudokoa maandazi manne, Jumapili ya Februari 12, 2023.

Baada ya mwalimu kumtuhumu akashirikiana na walinzi kuzuia mlango na dirishani ili mwanafunzi asiweze kutoroka, baada ya hapo wakaongezeka Walimu na kisha kuanza kumshambulia kwa kipigo.

Kipigo hicho kilisababisha majeraha makubwa kwenye mwili wa Mwanafunzi ndipo akapelekwa hospitali kwa ajii ya matibabu.

Baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi huyo amelazwa inadaiwa Walimu wakageuza kibao na kudai mwanafunzi ameumia wakati akiruka dirishani baada ya tukio la wizi wa maandazi.

Taarifa ya kutoka Hospitali
Vyanzo kutoka Hospitali zinaeleza kuwa hali ya Mwanafunzi siyo nzuri na amelazwa tangu Jumapili, anasaidiwa na baba yake mzazi ambaye ndiye anayemuuguza hospitalini hapo.

Shule yamtaka mzazi alipe hasara
Chanzo kutoka shuleni kinaeleza kuwa licha ya kinachoendelea, shule imegeuza kibao na kumtaka baba wa mwanafunzi huyo alipe gharama za kioo cha dirisha ambacho wanadai mwanafunzi alikivunja wakati akitoroka baada ya kuiba maandazi.

Tamko la Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amesema: “Nimebanwa na shughuli nyingine za kiofisi, nina wageni, lakini ninawaagiza Wasaidizi wangu wafuatilie kisha kama kuna tukio la aina hiyo tutatoa taarifa rasmi.

Ofisi ya Afisa Elimu
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju alipoulizwa kuhusu tukio hilo, amesema anaombwa atafutwe baadaye kwa kuwa ametuma wasaidizi wake kwenda kufuatilia.

Muuguzi wa Hospitali aeleza
Mmoja wa wauguzi wa kike ambaye amempokea mgonjwa huyo amesema “Aliletwa hapa akiwa hayupo vizuri kiafya, ana majeraha yanayoonekaa ni ya kupigwa eneo la uso, mguuni na mikononi.

“Anahudumiwa na baba yake ambaye ndiye anayemsaidia kumuogesha na kumpa huduma nyingine ambazo ni za binafsi sana.”

Aidha ameongeza "Kuna maofisa kadhaa nadhani ni kutoka ofisi ya Afisa Elimu, naona wamefika hapa na kumtafuta huyo kijana."

Tamko la mganga mkuu
Akizelezea hali ya mgonjwa, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ifisi, Dkt. Hamis Bakari Ally anasema: “Mgonjwa anaendelea vizuri, hali yake ni vizuri kiasi, ana maumivu ya mguu kwenye goti, ameeleza aliumia wakati anaruka kutoka kwenye chumba alichofungiwa, hali ya kichwa ipo sawa, hakuna mvunjiko wowote.

“Hivyo majeraha mengine aliyonayo yalitokea wakati aliporuka kutoka kupitia dirishani wakati akijaribu kutoka kwenye chumba alichofungiwa.

“Watu wa shuleni kwake ndio waliomleta, kuhusu gharama za matibabu ana bima ya NHIF ndiyo anaitumia.”

Alipoulizwa kuwa kama chanzo ni kushambuliwa kwa vipigo kutoka kwa Walimu na Walinzi kama inavyodaiwa, Dkt. Hamis amesema: “PF3 ipo, tunayo kwenye faili letu la hospitali."

Kuna tamko lolote kutoka shuleni au kwenye mamlaka?
Dkt. Hamis: “Hapana hakuna tamko lolote kutoka shuleni, zaidi maafisa wa ofisi ya Afisa Elimu wamefika hapa na kumuona mgonjwa kisha wakasema wanaendelea na uchunguzi wao wa ndani kwa ndani."

Je, ni kweli mwanafunzi alidokoa maandazi?
Dkt. Hamis: "Tumezungumza naye mwanafunzi kwa kuwa sisi madaktari huwa tunauliza chanzo cha majeraha, amesema ni kweli aliiba maandazi kwenye kiduka cha shule, kwa kuwa alikuwa na njaa, ndipo akakamatwa. Mwanafunzi mwenyewe anasema alipoona adhabu imezidi ndipo akaruka dirishani ili kukimbia na ndipo majeraha yakaongezeka."

Pia soma:
- Mbeya: Mwalimu anayetuhumiwa kumshushia kipigo Mwanafunzi aliyedokoa maandazi ashikiliwa na Polisi
 
Kuna mwalimu mmoja hapa anawaambia watoto waende kula Bata bichi. Yaani ticha anahubiri Bata, nanaenda na mkoba wake darasani umekaa vipodozi na anawapa watoto wambebee Mana unakuwa mzito mno.

Mara anadai siku hizi matak00 yanaitwa wowowwooo, kweli jamani hizi ndio taaluma za mwalimu.
 
Hawa walimu kwani hawakusikia yaliyomkuta mwenzao.

Hivi kumpiga mtoto kipigo kama mwizi inasaidia nini zaidi ya kuhatarisha ajira na usalama wako. Mtoto kakosa tafuta adhabu ngumu mpe ukiona haitoshi akapumzike nyumbani na wazazi wake.

Hata kama kaiba ila sio kumpiga hivyo.

Hawaoni wenzao wengine wanaishia jela au kufukuzwa kazi kwa ujinga huu huu na bado wanauendeleza.
Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Kuna haja ya mmoja ya walimu design ya hawa kuonyeshwa mfano na wazazi. Akamatwe na apigwe makonde ya haja. Nahisi hapo watapata msg kuwa mtoto wa mtu hapigwi kizembe.
 
Enyi walimu huko mbeya hamna mashamba? Hamna tution? Hamkumsikia RC mstaafu wa mkoa wenu?

Hiyo mitoto iacheni tuu tuzalishe taifa la freva, kwani mkiwa na matoto majizi shuleni au shule nzima wakipata sifuri nyie hamlipwi mshahara?

Ona sasa mmejiimgiza kwenye makucha ya wana siasa
ideot
 
Enyi walimu huko mbeya hamna mashamba? Hamna tution? Hamkumsikia RC mstaafu wa mkoa wenu?
Hiyo mitoto iacheni tuu tuzalishe taifa la freva, kwani mkiwa na matoto majizi shuleni au shule nzima wakipata sifuri nyie hamlipwi mshahara?
Ona sasa mmejiimgiza kwenye makucha ya wana siasa
ideot
Hujawahi ibiwa maandazi ndiyo maana unasema hivyo.
 
Back
Top Bottom