DOKEZO Mbeya: Mwanafunzi alazwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Rohila, inadaiwa alidokoa maandazi manne

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mleta mada bana

Naona unajaribu kukuza tukio ili walimu waonekane ndio tatizo.

Kwa maelezo yako umedai ni kweli mtoto aliiba,na ni kweli mtoto alipita dirishani. Na ni kweli walimu walimpiga

Lakini je hayo majeraha ni ya viboko?au ni kajikata na kioo na kufika chini vibaya ndipo akaumia?

Hapo mleta mada kuna vitu unajaribu kuviweka pembeni kwakua tu pengine unataka kuona walimu wanachukuliwa hatua au mhusika ni ndugu yako au walimu waliwahi kuku adabisha ukawachukia.

Kwanza huyo mtoto anaonekana ni mtukutu,kitendo tu cha kuiba mandazi sio ishara nzuri na kitendo cha kuruka dirishani inaonesha kabisa kuna tatizo mahali
 
Maadili jamani maadili, angekuwa mtaani Wananchi wenye hasira kali wangemmaliza
Wewe ni mwalimu katili pia? Maadiligani kwa hayo maandazi?? Tia ndani hao walimu na wasiruhusiwe kufundisha shule yoyote in TANZANIA kenge hao.
 
Kuna haja ya mmoja ya walimu design ya hawa kuonyeshwa mfano na wazazi. Akamatwe na apigwe makonde ya haja. Nahisi hapo watapata msg kuwa mtoto wa mtu hapigwi kizembe.
Mwizi lazima anyoshwe. Amevunja kabisa duka. Hawa ndio wakikua wanakuwa majambazi.
 
Wewe ni mwalimu katili pia? Maadiligani kwa hayo maandazi?? Tia ndani hao walimu na wasiruhusiwe kufundisha shule yoyote in TANZANIA kenge hao.
Hakuna kesi hapo, chuki yako ni kubwa sana
 
Bora hivyo kuliko kudeal na watoto watukutu,wananifurahisha sana walimu wa mkoa wa Dar.

Wameachana na habari za kusumbuana na watoto wa watu,wao wanafundisha tu basi.

Kuhusu nidhamu watajuana na wazazi wao na dunia. Matokeo yakija hovyo ni mzazi ndio atahangaika na mwanae kwa aman kabisa
 
Kuna kitu hakiko sawa kwa hawa walimu wa miaka hii,maana naona hizi kesi za wanafunzi kupigwa mpaka kupitiliza zimezidi sana...
 
Hata panya road walianzia kwny maandazi

Hayo majeraha kayapata kwa kuvunja kioo na kujaribu kutoroka chumban alikofungiwa kupita dirishani

Huyu mtoto Yuko kwny stage za awali za ujambazi, sio ujasiri wa kawaida huu.

WAZAZI TUSIFUGE VITENDO HIVI
 
Soma vizuri hapo juu, dogo aliiba na akachezea bakora ,baada ya kufungiwa room dogo ndio akavunja dirisha na hapo ndipo alipopata hayo majeraha ya mguu na usoni.

Sasa ndio ujue huyo ni mwanafunzi wa aina gani
Huyu dogo Ni jambazi ajae,
Ujasiri wa kuvunja kioo kupita dirishani Ni hatari Sana, huyu hata nyumba anavunja.
 
Kweli aisee,
Walimu wa Hapa wako bize mishe zao
Watoto Hizi shule za kata wanafeli mno[emoji26]
 
Sasa hao ndio magaidi huwa mnahangaika tu

Mandazi 4 mnataka kumtoa roho mtoto
Yaani adhabu zifutwe tu mashuleni maana hao sio waalimu siku hizi bali ni vibaka na majambazi na wazinzi

Enzi zetu unachapwa a mtu mzima kama baba na anakuchapa kwa kukufundisha ila sio hawa magaidi

PM futa ushenzi huu au tutaua bure
 
Lets call a Spade a Spade...

Alidokoa au aliiba; yaani ni Mwivi ?

Huenda wanajaribu kumkunja angali mbichi....
 
Hayo maandazi manne unayaona machache lakini ingekuwa kayaiba uraiani wenda yangesababisha kifo chake.

Na huyo kijana anavyo onekana amesha kuwa sugu huu ujasiri wa kuvunja dirisha ili atoroke ni wa hali ya juu sana.
 
Duuuuuuh maandazi manne ndio yana watoa utu kiasi hicho? Au kuna mengine nyuma ya pazia?
Na hapo ashukuru mungu tu ameyaiba kwenye duka la shule angekuwa kayaiba uraiani sasa hivi wazazi wangekuwa wana andaa ratiba ya mazishi.
 
Hivi hospital za Tanzania hawawezi kufunga majeraha vizuri kwa upendo? Ona hilo li gozi sijui pamba hapo kichwani... it's terrible
Hizo ndio hospital za government wanaharaka kinoma noma, wakute kwenye stitching ndio utajua kuna changamoto kwenye huduma hasa government
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…