Mbeya: Mwanafunzi amtia Mimba Mwanafunzi mwenzake

Mbeya: Mwanafunzi amtia Mimba Mwanafunzi mwenzake

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Kijiji Cha Kilambo ambaye ni Mwanafunzi wa kidato Cha nne katika shule ya Sekondari Ikimba Wilayani Kyela amehukumiwa kifungo Cha nje Cha miezi 12 pamoja na faini ya kiasi Cha shilingi laki mbili Kwa kosa la kubaka na kumpa Mimba Mwanafunzi mwenzake.

Jukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya wilaya Kyela na Mhe.Hakimu Paul Barnabas .

Hukumu hiyo ni Kwa mujibu wa kifungu Cha 130 kifungu kidogo Cha kwanza na Cha pili (e) na kifungu Cha 131 kifungu kidogo Cha pili (a) vyote vya Sheria ya kanuni ya Adhabu pamoja na kifungu 60 A kifungu kidogo Cha tatu Cha Sheria ya elimu.

Mshitakiwa alitenda kosa hilo Julia 15 2024 baada ya kumlaghai Mwanafunzi mwenzie kuwa atamuoa baada ya kumaliza masomo yake.
 
Madenti wengi hua wanapeana mimba wao kwa wao.

Sometimes inatokea binti akihisi ana mimba na kuna njemba ya mtaani kama ilikua inamsumbua sumbua binti anajileta kirahisi unakula unapewa zigo la miaka 30 ulibebe...
 
Mbona adhabu ndo Sana hio

Mbona adhabu hiyo ni kubwa sana, wote ni under 18!! au neno kubaka limekuchanganya? kufanya mapenzi na binti yeyote wa chini ya 18 ni kubaka, haina maana alitumia nguvu ndio maana wamefafanua alimlaghai kwa kumwambia atamuoa baada ya masomo.

Wototo zaidi ya asilimia 50 mashuleni huko wanafanya mapenzi, mtawafunga wangapi 😂😂
 
Back
Top Bottom