John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Okay,Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Kijiji Cha Kilambo ambaye ni Mwanafunzi wa kidato Cha nne katika shule ya Sekondari Ikimba Wilayani Kyela amehukumiwa kifungo Cha nje Cha miezi 12 pamoja na faini ya kiasi Cha shilingi laki mbili Kwa kosa la kubaka na kumpa Mimba Mwanafunzi mwenzake.
Jukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya wilaya Kyela na Mhe.Hakimu Paul Barnabas .
Hukumu hiyo ni Kwa mujibu wa kifungu Cha 130 kifungu kidogo Cha kwanza na Cha pili (e) na kifungu Cha 131 kifungu kidogo Cha pili (a) vyote vya Sheria ya kanuni ya Adhabu pamoja na kifungu 60 A kifungu kidogo Cha tatu Cha Sheria ya elimu.
Mshitakiwa alitenda kosa hilo Julia 15 2024 baada ya kumlaghai Mwanafunzi mwenzie kuwa atamuoa baada ya kumaliza masomo yake.
Ila Sheria inapaswa kubadilishwa ili Kama Mtuhumiwa wa ubakaji wa jinsia ya kiume anapotiwa hatiani, na mwanamke mhusika naye pia atiwe hatiani na kisha huyo mwanamke naye ahukumiwe angalau Nusu ya adhabu ambayo Mwanaume anahukumiwa nayo.
Mathalani, kama Mwanaume anahukumiwa kifungo cha jela miaka thelathini (30) Basi na Mwanamke naye ahukumiwe Nusu ya kifungo hicho, yaani apewe kifungo cha miaka kumi na Tano (15) gerezani. Hii itasaidia kutoa fundisho kwa wote kabisa