Mbeya: Polisi waandaa mafunzo maalum kwa madereva wenye leseni lakini hawakupita vyuo vya udereva na wasio na leseni

Mbeya: Polisi waandaa mafunzo maalum kwa madereva wenye leseni lakini hawakupita vyuo vya udereva na wasio na leseni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Picha 03.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga akiwa katika Stendi ya Mabasi Kabwe Jijini Mbeya, amezindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kimkoa kwa kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto, magari, pikipiki na bajaji pamoja na kubandika Stika za nenda kwa usalama barabarani.

Picha 02.jpg

Akizindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani kimkoa, Kamanda Kuzaga amewataka madereva wa Pikipiki, Bajaji, Magari madogo na magari ya abiria kuhakikisha vyombo vyao vya moto zinakaguliwa na wakaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi waliopo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuangalia ubora wake na kama vina sifa ya kutembea barabarani.

Aidha, ameeleza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya na wakuu wa vyuo vya udereva mkoa wa Mbeya wameandaa mafunzo maalum ya wiki moja kwa madereva wenye leseni lakini hawakupita katika vyuo vya udereva pamoja na wale ambao hawana leseni ili waweze kujifunza na hatimaye kupata cheti cha udereva kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali.

Naye, Mwenyekiti wa Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Eng. Rajab Ghulika amewataka madereva kujitokeza kuhudhuria mafunzo ya udereva ili kuwajengea uwezo na umahiri wa matumizi ya vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kujikumbusha alama na michoro mbalimbali ya usalama barabarani.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani imeambatana na ukaguzi wa vyombo vya moto, ubandikaji stika za nenda kwa usalama, utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara Pamoja na utoaji wa mafunzo maalum ya udereva kwa madereva na utoaji vyeti vya udereva kwa wahitimu. Kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitafanyika Aprili 20, 2023 katika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.
 
hili zoezi la mafunzo wangelifanya mikoa yote lingekuwa na manufaa zaidi.
 
Ila sio na lengo la wao kupiga hela.yaani sijui unanielewa Mana everything people are trading.huwa Kuna hidden motives kwa kila kinachofanywa mbele ya macho ya watu. Ni sawa ukawa chawa ukaanza heshima sio kuwa Ni free Bali inaharibu ku trade your respect with other benefits
 
Kama waalimu wa vodafasta?

Kwa hivyo mafunzo ya udereva kwenye vyuo maalum yanachukua zaidi ya mwezi bila sababu ya msingi?
Inafikirisha kwakweli.
 
Back
Top Bottom