Mbeya: Polisi wamshikilia Diwani na wenzake kwa kumpiga mpiga picha

Mbeya: Polisi wamshikilia Diwani na wenzake kwa kumpiga mpiga picha

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mnamo tarehe 03.03.2022 majira ya saa 08:00 asubuhi huko Mtaa wa Igodima, Kata ya Iganzo, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya, Kijana aitwaye SHADRACK ZACHARIA [28] Mpiga Picha na Mkazi wa Igodima Jijini Mbeya anayeonekana kwenye “clip” ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii akishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na viongozi wa Kata ya Iganzo kwa kile kinachoelezwa ni kutoa lugha ya matusi na kuwapiga picha bila idhini yao wakati wakifanya shughuli za maendeleo katika Mtaa wa Igodima.

Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na kukataa kutoa eneo kwa ajili ya kupitisha njia ya mtaa.

Awali, mama wa mhanga aitwaye ESTHER ANDREW [58] Mratibu Elimu Kata na Mkazi wa Igodima kabla ya kununua eneo hilo wakazi wa eneo hilo walikuwa wanapita njia lakini baada ya kununua na kujenga nyumba aliziba njia, ndipo wakazi wa mtaa huo walifika ofisi za kata kutoa malalamiko ambayo yaliamuliwa kwenye kikao kuwa kila upande utoe hatua moja ili kupitisha njia ya mtaa.

Hivyo siku hiyo ya tarehe 03.03.2022 asubuhi Diwani wa Kata akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Mtaa na wananchi walifika hadi eneo husika na kuanza kuchonga barabara ndipo ugomvi ulitokea.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watuhumiwa watatu kwa mahojiano ambao ni:-
1. DANIEL WILLIAM [35] Diwani wa Kata ya Iganzo.
2. ERASTO MWANKENJA [48] Afisa Mtendaji Kata ya Iganzo.
3. HENJE MBOMBO [74] Mkazi wa Iganzo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalaani tukio hilo na linatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watafute suluhisho la migogoro yao kwa kufuata njia zilizo sahihi ikiwa ni pamoja na kuvihusisha vyombo vya haki likiwemo Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutofuata sheria.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
 
Kupiga picha bila idhini ni dhana mfu, si kila picha za matukio ni lazima uombe idhini picha zingine hupigwa katika mazingira magumu na hatari na habari zake zinapaswa umma kujua
 
Sasa huyo Mwananchi anazibaje barabara kuzuia wenzake kupita? ni akili matope uanze kugombana na Kijiji kizima kisa ujuaji na Uanaharakati usio na maaaana. Akili za WanaVijiji huko Mikoani wanazijua wenyewe, huyo awe mpole aruhusu barabara ipite maisha yasonge mbele vinginevyo ndiyo mara nyumba imewaka moto, oooh nina mikosi, oooh viffo vya Utata, Hebu tuwe waungwana pindi tnapokaribishwa mahala. Hapa mtandaoni mtampa bichwaaaa lkn hukp field ataishia pabaya ni huu ujuaji wake.
 
Back
Top Bottom