Mbeya: Radi yaua watu watano wa familia moja

Mbeya: Radi yaua watu watano wa familia moja

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
images.jpg

Watu watano wa Familia moja Wakazi wa Kitongoji cha Nkangi kilichopo Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamefariki dunia kwa kupigwa na radi usiku wa kuamkia leo December 29,2024 wakiwa wamelala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Watu hao watano wa Familia moja ya Masiganya Scania (39) ambaye ni Mfugaji walifariki dunia baada ya kupigwa radi kwenye
kambi ya kuchungia ng’ombe wakiwa wamelala.

Waliofariki katika tukio hilo ni Balaa Scania (28), Kulwa Luweja (17]), Masele Masaganya (16), Hema Tati (10) na Manangu Ngwisu (18) .

“Katika tukio hilo Watu wengine watano walijeruhiwa ambao ni Gulu Scania (30), Manyenge Masaganya (13), Seni Solo (13), Paskali Kalezi (16) na Huzuni Kalezi (19), chanzo cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha usiku ikiambatana na radi, Majeruhi walkimbizwa katika Kituo cha Afya Isangawana kwa matibabu na walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali zao kuwa nzuri”
 
Back
Top Bottom