The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ulianzishwa kwa lengo la kunusuru kaya masikini na kusaidia wananchi wasiojiweza wakiwemo wazee.
Baada ya kufikiwa na mpango huo kwa baadhi ya wananchi waliopo kijiji cha Shibolya kilichopo wilaya na Mkoa wa Mbeya ulionekana kuwa msaada mkubwa katika kuzikwamua kaya masikini kiuchumi kutokana na ufanisi na mipango iliyokuwepo.
Mambo yalianza kubadilika taratibu baada ya kundi kubwa la wanufaika wa mpango huo kuanza kuondolewa na ili kurudishwa katika mpango huo likawekwa sharti la kuwa ni lazima wanufaika wafanye kazi za mikono ndipo watakapopata fedha za TASAF.
Hali hiyo imekuwa ni kama mateso kwa baadhi ya wasiojiweza hasa wazee ambao wanalazimishwa kufanya kazi ngumu kama uchongaji na utengenezaji wa barabara. Unawezaje kumbebesha kifusi mzee mwenye umri wa miaka 75, 80 wanabebeshwa Koleo na majembe ili wakatengeneze barabara ndiyo wapate fedha hizo.
Serikali imeshindwa kutengeneza barabara na sasa wanatumiwa wazee wasio na nguvu kutengeneza barabara ndiyo wapate hela za TASAF.
Huku ni kuhatarisha afya za wazee, serikali izuie wazee kufanyishwa kazi nzito kwa ndipo wapate fedha za TASAF ili kuzuia kudhoofisha afya zao.