Kinachonisikitisha ni hulka ya watawala wetu kukimbilia kufungua vyuo vikuu vingi bila kwanza kuboresha mazingira ya kupatikana elimu ya kiwango kinachotakiwa. Bado vyuo vikuu vingi vinaupungufu wa vifaa, maabara na rasilimali watu (Lecturers and Technicians). Pili kinachoniudhi zaidi ni kuvichukua hivi vyuo ambavyo vilikuwa vinafundisha watendaji muhimu kwenye nyanja mbalimbali. Hivi vyuo vya UFUNDI ama vinavyotoa CERTIFICATE and DIPLOMA ni muhimu sana, kwani elimu inayotolewa na vyuo hivi haipo kwenye ma-universites yetu. Hulka hii imepelekea pia kushusha kiwango cha kuingia vyuo vikuu, na hili limepelekea kushuka sana kwa elimu yetu. Wanafunzi wengi ambao ndiyo wange-qualify for Diploma studies sasa wanaingia Vyuo vikuu moja kwa moja, na sasa tutegemee pengo kubwa sana kwa technicians/watendaji wa ngazi za diploma sababu tu ya kutokuwa na focus nzuri.