Mbeya Universit Of Science and Technology

Mbeya Universit Of Science and Technology

Joined
Aug 22, 2011
Posts
49
Reaction score
7
Leo kwenye Mkutano mkuu wa Chama cha CCM wamekipandisha hadhi kilichokuwa chuo cha ufundi Mbeya kisha taasisi ya Science na Technology hatimae Mbeya Universit of Science and Technology, Ni hatua nzuri sana kusikia hivyo hususani kwa sisi tuliosoma pale miaka ya 2002 kuendelea.Shida ni kukitunuku chuo kwenye Mikutano y'a Chama Cha siasa ,Sijui mnasemaje...? Shughuli za Serikali zikihusishwa kwenye Chama.
 
Jamani tangu lini suala la kitaaluma likafanyika kisiasa? Nini nafasi ya TCU? Sheria itabadilishwa lini na pia lazima pia kuweko vyuo vinavyotoa elimu kwa kada za chini hasa DIPLOMA ili kupata technicians. Kama kila chuo kitakuwa Univesrity Kutakuwa na shida huku tuendako? VETA bado haikidhi mahitaji vile vile Arusha Tech.
 
Kinachonisikitisha ni hulka ya watawala wetu kukimbilia kufungua vyuo vikuu vingi bila kwanza kuboresha mazingira ya kupatikana elimu ya kiwango kinachotakiwa. Bado vyuo vikuu vingi vinaupungufu wa vifaa, maabara na rasilimali watu (Lecturers and Technicians). Pili kinachoniudhi zaidi ni kuvichukua hivi vyuo ambavyo vilikuwa vinafundisha watendaji muhimu kwenye nyanja mbalimbali. Hivi vyuo vya UFUNDI ama vinavyotoa CERTIFICATE and DIPLOMA ni muhimu sana, kwani elimu inayotolewa na vyuo hivi haipo kwenye ma-universites yetu. Hulka hii imepelekea pia kushusha kiwango cha kuingia vyuo vikuu, na hili limepelekea kushuka sana kwa elimu yetu. Wanafunzi wengi ambao ndiyo wange-qualify for Diploma studies sasa wanaingia Vyuo vikuu moja kwa moja, na sasa tutegemee pengo kubwa sana kwa technicians/watendaji wa ngazi za diploma sababu tu ya kutokuwa na focus nzuri.
 
Mawazo mazuri....!
 
naomba niwaambie ki2,chuo kimetunukiwa hadhi yakuwa chuo kikuu hiyo imepiganiwa toka cku nying mno mpk leo hii wamefanikisha,nihivi watu wa diploma (technicians) wanaendelea kuwepo daima na daima kama mwanzo pamoja nakupandishwa hadhi so ondoeni hofu juu ya hilo, diploma students and bachelor students also masters degree programme vyote vitakuwepo,hakuna kitakachomic au vp
 
HAKUNA UBISHI,kutoka MTC,MIST na sasa MUST chuo hicho kinastahili,na PLAN za kukiweka chuo hicho kuwa univ ni za muda mrefu sana.
Kwa ninavyojua swala hilo lishaamuliwa muda kidogo, CCM kama chama tawala na sera zake ndo zinazoendesha nchi hii ilikuwa haina tatizo kulizungumzia swala hilo katika kikao chao kama mafanikio ya mipango yao,na sio kama maamuzi ya kuwa univ yalifanyika pale.LAH
 
Back
Top Bottom