Mbeya: Viongozi wa Bajaji Mbeya Jiji tuacheni na Abiria wetu tunajuana wenyewe

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
879
Reaction score
814
Hivi ninyi viongozi wa Bajaji jiji la Mbeya mna matatizo gani?

Sawa tumekubaliana kuwa madereva wote wa Bajaji tubebe Abiria Kwa nauli ya shilingi 800 kituo Hadi kituo,Sasa Kuna shida gani kama Abiria ameniomba Kwa shilingi 500.

Maana mnatangaza kabisa eti mkitukamata tukiwa tunachukua nauli za shilingi 500 mnatupiga faini.

Kwani ninyi viongozi mnaumia na Nini sisi tukibeba Abiria Kwa nauli ya shilingi 500?

Hii ni biashara huria hivyo mtuache tuendelee na kazi yetu,kama Kuna dereva anaona mia tano kwake ni ndogo aache tuwabebe sisi ambao tumetumwa kutafuta pesa.

 
Ina kitu utafika mbali
 
Hii nimeiona Mbalizi, Bajaji mna Viranja kama sekondari, yaani abiria kutoka Tarafani hadi ZZK analipa sawa na abiria kutoka Tarafani hadi Ifisi..
Tatizo hawo viongozi na hizo katiba mnapitisha nyie wenyewe, kwenye vikao vyenu sisi abiria hatuwepo
 
Mkifika 800, daladala zitaweka 500

Abiria atachagua sasa
 
Na nyie bajaji punguzeni vurugu barabarani na waongeze barabara na kupanua barabara kuu.

Watu wanakimbilia bajaji kwasababu ya foleni.
 
Siobajaji tuu kuna wengine wanajiita umoja wa library...
Hawa nao kama wamama wa kausha damu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…