POTOSHI Mbeya wanachama CHADEMA wameandamana kuwa Heche awapishe, hawamtaki

POTOSHI Mbeya wanachama CHADEMA wameandamana kuwa Heche awapishe, hawamtaki

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa inaonesha baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakiandamana kupinga uwepo wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche.

Video hiyo imeambatana na ujumbe unaosema:"CHADEMA wamefanya maandamano makubwa wakitaka Makamu Mwenyekiti wao, John Heche, ajiuzulu kutokana na tuhuma za wizi wa fedha za chama."

Je ni upi uhalisia wa video hiyo?

1785745426555.png
 
Tunachokijua
Kumekuwa na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa ni maandamano ya wanachama wa CHADEMA wakimtaka Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, John Heche.

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa hakuna uthibitisho kuwa video hiyo ya watu wanaonekana kuandamana kuwa yalikuwa ni maandamano ya kumtaka Heche awapishe huku mkoani Mbeya.

Kipande hicho kimechapishwa Agosti 2, 2026 katika mtandao wa Facebook lakini ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za revesrse image search imebainika kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni kabla ya Agosti 02, 2026.

Mathalani mtumiaji mmoja wa mtandao wa Youtube alichapisha kipande hicho cha video Julai 7, 2026. Baadhi ya wachangiaji katika video iliyochapishwa AGosti 02 walitoa maoni yao kuwa wao wapo mkoani Mbeya lakini hakuna maandamano hayo.

Hata hivyo sauti watu wanaoimba kwenye maandamano hayo haioneshi kuwa wanaimba kumtaka John Heche awapishe kwenye chama hicho.
Back
Top Bottom