the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Kikundi cha Wanawake SHUJAA Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamchangia Fedha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya Milioni Moja kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais, ikiwa ni kumuunga mkono katika jitihada zake za uongozi.
Zoezi hilo limeongozwa na Dkt. Yasinta Mafwenga ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wanawake la kujikwamua kiuchumi.
Wanawake hao wamesema wamefikia hatua baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia, ambapo katika Wilaya ya Rungwe, huduma za afya na maji zimeimarishwa kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya vituo vya afya vilivyojengwa katika Wilaya ya Rungwe ni pamoja na Kituo cha Afya Ikuti, Masukulu, Isongole na Mpuguso.