Mbeya: Watu watatu Wafariki na wengine tisa wajeruhiwa katika ajali ya gari na bajaji

Mbeya: Watu watatu Wafariki na wengine tisa wajeruhiwa katika ajali ya gari na bajaji

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1732731848908.png

Watu kadhaa ambao idadi na majina yao hayajajulikana wanahofiwa kufariki dunia baada ya ajali iliyohusisha magari matano, bajaji nne na pikipiki moja eneo la Mbembela jijini Mbeya.

Ajali hiyo imetokea leo Novemba 27, 2024 ambapo mpaka sasa vyombo vya ulinzi na usalama na uokozi tayari vimefika eneo la tukio.

Hii ni ajali ya pili kwa kipindi cha miezi miwili tangu ilipotokea iliyoua zaidi ya watu 10 na kujeruhi wengine kadhaa.


WATU watatu wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa , katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Mbembela, Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, ajali hiyo ilitokea Novemba 27, 2024 majira ya saa 12 jioni, kwenye barabara kuu ya Mbeya-Tunduma.

Kamanda Kuzaga amesema lori namba T.537 DNC aina ya FAW, lililokuwa na tela namba T.241 ARG, likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoani Songwe, likiwa limebeba madini ya Sulphur, lilipoteza uelekeo na kugonga magari sita, bajaji nne, na pikipiki moja.

Ameyataja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T.199 DYF Toyota Coaster, SU 44682 Toyota Double Cabin mali ya Shirika la Posta Mbeya iliyokuwa ikiendeshwa na Fredy Mwasanga (48), mkazi wa Soweto, gari T.134 DXK Toyota Double Cabin, iliyokuwa ikiendeshwa na Lusekelo Mwaseba (48) mkazi wa Sae, Gari T.370 ABN Toyota Land Cruiser, gari T.344 BTS Toyota Cresta na gari T.474 EHL/t.449 EHL aina ya FAW iliyokuwa ikiendeshwa na Alon Ruben (50) mkazi wa Isanga.

“Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu watatu, wawili wakiwa wanaume na mmoja wa kike, na majeruhi tisa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,” amesema Kamanda Kuzaga.
 
Nilitaka niulize watu wamekufa wangapi?
Maana walivyoanza kuwanyofoa mi nikakimbia😭

Maisha hayana maana
Kumbe uko mbeya mkuu ,tuonane bwana twende kunywa hata ulanzi Mafiati ,nasikia Kuna dada mtanga amefungua glocery anakuwa na ulanzi kutoka Iringa kila jumamosi .

Dah ajari hizi ,Mungu atuepeushe.
 
Mjin iwe ni marufuku kwenda mwendo wa zaidi 50, kuwe na fine kubwa kuliko ile ya afu 30.

Kuna wajinga wanakimbia na maghari unashindwa kuelewa shida nin
 
Mwisho wa mwaka huu

Watu wamwombe sana MWENYEZI MUNGU shetani yuko mawindoni
 
Back
Top Bottom