LGE2024 Mbeya: Yaliyotokea Serikali za Mitaa bado ni kidonda kwa CHADEMA

LGE2024 Mbeya: Yaliyotokea Serikali za Mitaa bado ni kidonda kwa CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Mbeya kimesema Serikali imekuwa chanzo cha kuruhusu mianya ya wizi wa chaguzi zinazofanyika kwa kuwaondoa wagombea wa upinzani ili kukipitisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo kuunga mkono mpango wa kuwa bila mabadiliko ya mifumo ya kiuchaguzi basi uchaguzi mkuu usifanyike.

Hata hivyo, Chama hicho kinadai kuwa hakiko tayari kutoa mawakala wake kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura wala kuwapa ushirikiano wowote kutokana na kuvurugwa kwa uchaguzi uliopita wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kikidai kilichofanyika ni hujuma ambazo zisipotafutiwa ufumbuzi zitajirudia kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa tarehe 23 Desemba, 2024, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya, Christopher Njelenje amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na Serikali wameweka mazingira magumu kwa wapinzani, hivyo kuwaibia ushindi wapinzani hali anayodai hawatavumilia mpaka yafanyike mabadiliko ya kiuchaguzi ikiwemo Tume huru ya uchaguzi kupatikana ili wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Naye, Katibu wa CHADEMA jimbo la Mbeya Vijijini, Pess Mapunda amesema maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA ya 'No reform no election' ni sahihi na wako tayari kuyaunga mkono kutokana na maumivu waliyoyapitia kwenye chaguzi kadhaa zilizopita.

Wanachama wa CHADEMA wamekemea wanachodai ni uporaji Demokrasia kwa kuwa na idadi ya viongozi ama wachache wa upinzani kwenye nafasi za Serikali za mitaa, vijiji, kata na Bungeni tofauti na hali ilivyokuwa kwenye chaguzi za nyuma ya mwaka 2015 wakitolea mfano katika jiji la Mbeya ambalo hakuna mtaa hata mmoja uliochukuliwa na Chama chao (CHADEMA) jambo wanalopinga vikali.
IMG_1965.jpeg
 
Acha bwana! Ni vile tu hujui kwamba Mbeya kuna wakala mkuu wa saccos nayetambuliwa na mmiliki wa saccos aliyepiganiwa kwa fedha za Abdul mpk akashinda.

Sijui umenielewa au niongeze sauti??
 
Back
Top Bottom