Mbezi iwe lango la jiji

Mbezi iwe lango la jiji

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Kutokana na ukweli kwamba stendi ya kimataifa imehamia mbezi na kwamba ndio njia pekee ya kuingia jijijini kwa mikoa yote ya nyanda za juu,kanda ya ziwa na kanda ya kati. Basi kuna kila sababu kuifanya mbezi iwe nzuri na ya kipekee.

Nchi zote za kusini mwa Afrika zinaingia jijini kupitia njia hii,hivyo Mbezi inatakiwa iwe ya kushangaza kwa uzuri na si kushangaza kwa uholela kama ilivyosasa mabanda hadi katikati ya barabara...vyoo vya mabati,vilabu vya pombe vya mabati, maskani za mateja,mamantilie n.k.

Hii ni aibu kubwa mno sehemu muhimu kama hii kuwa na miundombinu mibovu na holela kiasi hiki.

Mbezi inatakiwa mtu akifika aseme kweli nimeingia Dar es salaam, flyover za maana,malls za kutosha, gardens,biashara zenye mpangilio mzuri,sky scraper za kutosha na kila aina ya mbwembwe hadi mtu akifika apotee kwanza kisha ndio ajitafute.

Mbezi ya sasa ni aibu tupu kwa wenyeji na zaidi kwa wageni. Juhudi za makusudi zifanyike kupainua

Mifuko ya kijamii iliyokuwa na projects za kujenga majengo marefu wapewe ruhusa maalum kwa ajili ya kuijenga Mbezi.

Sio hadi wazungu waje watusaidie kufikiri vitu vidogo kama hivi. Juhudi za makusudi zifanyike
 
Mbezi yote ile ilitakiwa isawazishwe iwe tambarare zijengwe hotels,masoko makubwa, viwanja vya michezo,nk.kama mwanzo wa kuingia mji
 
Mbezi yote ile ilitakiwa isawazishwe iwe tambarare zijengwe hotels,masoko makubwa, viwanja vya michezo,nk.kama mwanzo wa kuingia mji
Mbezi yote isawazishwe? Imekuwa kiwanja cha 20x20? You must be joking I suspect!
 
Kwanini ilishindikane hali vifaa vipo
Kama kipande cha barabara kisichozidi upanda wa 10m na urefu usiozidi 10km kinachukua mwaka kusawazisha then kusawazisha eneo lote la Mbezi will take a century.
 
Kama kipande cha barabara kisichozidi upanda wa 10m na urefu usiozidi 10km kinachukua mwaka kusawazisha then kusawazisha eneo lote la Mbezi will take a century.
Inasikitisha kuona hata ile njia ya 8 kumalizia tu imekua ishu...hadi ianze kuharibika tena
 
Mbezi yote ile ilitakiwa isawazishwe iwe tambarare zijengwe hotels,masoko makubwa, viwanja vya michezo,nk.kama mwanzo wa kuingia mji
Yaani hata kusawazisha vile vichuguu pembeni ya barabara wameshindwa
 
Kama kipande cha barabara kisichozidi upanda wa 10m na urefu usiozidi 10km kinachukua mwaka kusawazisha then kusawazisha eneo lote la Mbezi will take a century.
Sio kweli,baruti zinafanya Kazi nzuri Sana siku nne tu usasawazisha.
Unapiga baruti kisha unaingiza bulldozer linapush kusukumiza bondeni kifusi pana kaa level.
 
Sio kweli,baruti zinafanya Kazi nzuri Sana siku nne tu usasawazisha.
Unapiga baruti kisha unaingiza bulldozer linapush kusukumiza bondeni kifusi pana kaa level.
Vichuguu vyenyewe vidogo halafu vichache...wanasawazisha kwa bulldozer tu chap
 
Back
Top Bottom