Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Ni takribani siku ya tano sasa wakazi wa Mbezi Juu, maeneo ya Makonde, Jogoo pamoja na mitaa ya Salasala hatupati huduma ya maji, huku DAWASA ikiwa haijatoa taarifa yoyote kuhusu changamoto iliyopo.
Wananchi wengi wanateseka na wameanza kuzunguka na vidumu mitaani kutafuta maji, jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa katika shughuli zao za kila siku.
Hatutegemei changamoto ya maji kudumu kwa zaidi ya siku tatu bila mamlaka husika kutoa taarifa kwa umma kuhusu kinachoendelea na hatua zinazochukuliwa.
Wito wangu, kwa niaba ya wananchi wengine ambao tunapitia usumbufu kutokana na changamoto ya kukosa maji, ni kwa DAWASA kutatua changamoto iliyopo na kurejesha huduma ya maji kwa wananchi.
Aidha, tunawaomba wajenge utamaduni wa kutoa taarifa kwa umma kwa wakati, ili wananchi waweze kufahamu endapo kuna mgao, hitilafu au sababu nyingine inayosababisha kukosekana kwa huduma ya maji.
Soma pia